Na Bashir Nkoromo, Tegeta
Jumapili ya Mei 8, mwaka huu (lango la 12 Abibu 1) ilikuwa siku nyingine ya kipekee kwa Kanisa Halisi la Mungu Baba, pale lilipofanya kwa mafanikio makubwa Mkutano wake Mkuu, ambao ulifanyika Makao Makuu ya Kanisa hilo, Tegeta Namanga, Jijini Dar es Salaam.
Moja ya Mambo yaliyofanya Mkutano huo kufana na hivyo kufanya siku hiyo iwe ya kipekee kwa Kanisa hilo, ni Kuhudhuriwa na maelfu ya Wajume kutoka nchi nzima na pia tofauto na mikutano mikuu ya Taasisi zingine ambayo wanaokubalika kushiriki huwa ni wajumbe halali tu Kikatiba, katika mkutano Uzao (waumini wa Kanisa hilo na Waalikwa wa kawaida waliruhusiwa kuushiriki mwanzo hadi mwisho.
"Sasa nataka niwaambie nilichowaitia, katika Mkutano huu wa habari njema. Ninyi mnajua katika mikutano ya wengine huwa ni patashika nguo kuchanika, lakini sisi mkutano wetu huu ni wa habari njema, kwa hiyo baada ya ibada hii uzao (waumini) na wote mliomo humu msitoke.
Kwa kuwa Kanisa hili ni la Kijamii, ninaruhusu hata msiokuwa wajumbe na waalikwa wa kawaida baada ya ibada hii mbakie humu ndani ili kila mmoja asikilize tutakachozungumza maana kinawahusu wote". Akasema Kiongozi Mkuu wa Kanisa hilo anayeitwa Baba Halisi, mwanzoni mwa Mkutano huo Mkuu.
"Heri, Heri", Baba Halisi akawasalimia Uzao (Waumini), nao wakaitika "Heriiiiiiii". Akaanza kufanya shukurani (maombi) ya kufungua Mkutano huo Mkuu, baada ya Ibada ya Kawaida kumalizika, kisha akasema, "Mimi nitaanza kwa kueleza mambo kama sita hivi, halafu nitampa nafasi Kuhani Moja aje hapa kueleza mambo yaliyofanywa na Kanisa hili ndani ya kipindi cha miaka minne cha uwepo wake hadi sasa".
Baba Halisi akazungumzia mambo kadhaa ikiwemo kuhusu mradi wa Kiwanda cha Maji cha 'One Up' ambacho Kanisa Halisi limekijenga eneo la Karege, Bagamoyo katika mkoa wa Pwani, akazungumzia pia hali ya Utawala wa Kanisa hilo na kuhusu fedha za matubda (Sadaka) ya kujenga moyo, akisema, "matunda ya kujenga moyo, kwa kuwa tulikuwa hatujafikia Uwanja wa Moyo ambao tumefika sasa, naona kama yalisuasua kidogo".
Akizungumzi kuhusu Kiwanda hicho, Baba Halisi alitumia zaidi ya dakika 30 kufafanua na kutoa darasa kwa waliohudhuria Mkutano Mkuu huo, hususan Uzao ili waelewe kwa kina mfumo bora utakaotumiwa na Kanisa hilo kusajili Kampuni itakayosimamia Kiwanda hicho, ili kila Uzao awe mmiliki bila kuvunja sheria za Usajili huo.
"Heriiiii, nimeona niwashirikishe yaliyoko mbele, maana naona wamekawia kidogo kuwaletea soda, haya yaliyopo mbele ni matamu kuliko tuliyofanya huko nyuma, na kwa kuwa nimewaambia kuwa hili Kanisa ni la Kijamii ndiyo nimesema wote mbakie humu ili myasikie tutakayozungumza maa maana yanawahusu wote", akasema Baba Halisi.
"Katika kusajili Kampuni hii kwa namna tunavyotaka, tumeona kuwa kisheria kuna 'complication' (changamoto), lakini Chanzo Halisi, ametusaidi kupata mfumo ambao 'utafiti' kwenye sheria zilizopo za kutoa kodi maana kama unazalisha lazima utoe kodi hapo hawawezi kukuhurumia usitoe kodi kwa kuwa eti wewe ni Kanisa, lazima utoe kodi kwa sababu unazalisha", akasema Baba Halisi na kuongeza;
"Sasa Sauti ilisema Uzao Halisi wote ni wamiliki, sasa kuna 'option' mbili, suala la kuanzisha Kampuni kama 'Ptivate Company' na suala la kuanzisha kama 'Public Company', lakini options zote hizi mbili kwa idadi tuliyopo zina 'Complication' ila Chanzo Halisi (Mungu Baba), ana uwezo ametusaidia kujua namna ya kufanya", akasema Baba Halisi.
"Ukitaka kuanzisha 'Private Campany' ni kuanzia watu wawili hadi 50, kwa jinsi tulivyo wengi ilitakiwa tuwe 'Public Company' lakini ina changamoto zake, ukishasema ni 'Public Company' mtu yeyote anaweza kwenda soko la hisa hata akiwa wa hovyo akanunua hisa, sasa hilo kwa kuanza itatusumbua kidogo.
"Sasa naomba niwape kitu ambacho Chanzo Halisi amenielekeza kufanya", Baba Halisi akasema, kisha akawaita mbele yake Makuhani kadhaa, akawambia kila mmoja ashike faili moja na kusema kwamba Makuhani hao walioshika mafaili ndiyo mfano wa Makuhani wa mikoa, na kufafanua akisema, "hivyo mnavyoona maana yangu ni kwamba kila Kituo kitatoa Uzao mmoja halafu ndiye aandikwe jina lake kwenye faili kisha wengine wawe nyuma ya huyo Uzao hata wakiwa 500".
"Hata Mataifa (Wasiokuwa Waumini wa Kanisa Halisi) wakipenda pia watasimama katika Taifa, maana 'limitation' kisheria kama ni 'Private Company' wapo 50, kwa hiyo yanatakiwa yawe mafaili ya Uzao 50 ila katika kila faili waandikwe hata 1,000. Sasa hiyo ndiyo itakayo-prove kwamba sisi ni familia au siyo familia", akafafanua Baba Halisi.
Katika kuhakikisha kila mmoja anaelewa, Baba Halisi akamsimamisha Kuhani mmoja wa Morogoro Dk. Paul, akawauliza Wajumbe wa Mkutano huo huku akitabasabu na kutoa kicheko kidogo, "Hivi kama huyo Dk. Paul anaweza kula fedha za uzao wengine? hamumwamini? Eeh hamumjui?" Baba Halisiakauliza nao wakajibu "tunamuamini".
"Enhee! Yaani maana yangu ni kwamba, huyu anatoka kituo hiki, na huyu kituo hiki, hivi mtu kama huyu mama aliyekuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili Tanzania, anaweza kula hela za wengie kweli?", kauliza Baba Halisi huku akiwaonyesha Uzao wamuone huyo Mama ambaye alikuwa miongoni mwa Makuhani walioambiwa kusimama mbele yake na kushika mafaili, kisha Baba Halisi akaendelea;
Sasa mmenielewa? Kwa hiyo ninyi wenyewe kwenye kituo ndiyo mtakuwa mnaangalia nani mnamwamini halafu ndiye ashike faili. Mumenielewa? Wajumbe walipomjibu kwa sauti za chini chini akawauliza, "mbona mnaitika kinyonge"? wakajibu "tumekuelewa".
"Mnajua nafafanua hivi ili muelewe vema kwa sababu lazima tuende kisheria. Halafu mwaka kesho tukikutana tena tutajua nani alikula fedha za mwingine nani hajala. hivi mnaamini kuna mtu atakula hela za mwingine? hiwezekani.", akasema Baba Halisi, kisha yeye na Wajumbe wakaangusha kicheko ukumbini.
Ili kuwathibitishia Uzao kuwa hakuna mwenzao yeyote atakayekula fedha zao, akaweka msisitizo kwa kusema, "Mimi hapa kabla hatujaanza, hawa nitawaapisha kiapo kikali sana, sana. Siajawahi kuapisha mtu yeyote ila hapo nitawaapisha, maana Kiwanda cha Maji ni chakula hivyo lazima kisimamiwe na waaminifu".
"Halafu upande mwingine lazima tuwe na Menejimenti ya Kiwanda, Wataalam tunao, hata ukitaka kuanzisha kiwanda cha soda wataalam tunao", akasema Baba Halisi.
Baada ya haapo Baba Halisi alizungumizia vituo vya Kanisa Halisi vilivyokwishajengwa ndani na nje ya Tanzania na ambavyo bado ujenzi wake haujakamilika hivyo akahimiza zipatikane fedha kukamilisha ujenzi na kununua viwanja vya kujengwa vituo vipya.
Kuhusu utawala wa Kanisa Halisi la Mungu Baba, Baba Halisi aliwaomba Wajumbe wa Mkutano huo Mkuu
Kumuidhinisha Kuhani Bubaberi kuwa Katibu wa Makao Makuu ya Kanisa hilo kwa ajili ya kusaidiana na Asteria Mlango ambyae kwa sasa anauguliwa na kichwa (Mume) wake.
Pia Baba Halisi aliwataka Makuhani kufanyakazi kidigitali badala ya kufanyakazi Kianalogia, ambapo aliwahimiza kuwa wanatuma nyaraka kwa 'sofy copy' kupitia simu janja na njia zingine za kielekroniki badala ya kutuma kupitia makaratasi.
"Mimi sina sekretari, hawa Vijana Kusudi na utawala wa Amani, muwe mnawatumia document kidigitali, na hata masuala ya fedha, nataka niwe napata ripoti kidigitali. Wewe tuma tu, ninachohitaji nataka niwe najua ili nikuinue (nikuombee) zaidi, sikunyang'anyi fedha zako, yaani nataka tuwe tunaonana kupitia mfumo wa 'C me C you', simnaujua mfumo huu au mauujui? Naomba mkubali hilo, tutabarikiwa", Baba Halisi akasema.
Baada ya Baba Halisi kumaliza akamualika Kuhani Moja kutoa ripoti yake ya masuala mbalimbali yaliyokwishatekelezwa na Kanisa Halisi la Mungu Baba katika kipindi cha miaka minne ya Kanisa hilo.
Wajumbe mbalimbali waliosheheni Ukumbini👇
Wajumbe, Makuhani na Uzao wa Dar es Salaam, wakiwa ukumbini tayari kumsikiliza Baba Halisi.
Mwalikwa aliyetambulishwa kwa jina la Imani (ambaye hakuvaa vazi jeupe), akifurahi baada ya kutambulishwa na Baba Halisi.
Baba Halisi akiendelea kutambulisha makundi mbalimbali
Kuhani Moja na Kanisa wake wakiwa kwenye Ibada na Mkutano huo Mkuu.Baba Halisi akifanya Shukurani mwanzoni mwa ibada iliyoutangulia Mkutano huo Mkuu.Baadhi ya makuhani wakipokea Shukrani iliyokuwa ikiendeshwa na Baba Halisi.
Mama Halisi akipokea Shukrani iliyokuwa ikiendeshwa na Baba Halisi.Uzao waliokuwa kwenye mahema maalum nje ya ukumbi wakipokea shukrani iliyokuwa ikiendeshwa na Baba Halisi.
Baadhi ya Wajumbe, Uzao na Makuhani wakipokea Shukrani iliyokuwa ikiendeshwa na Baba Halisi.Kaka Huduma Moja, akipapasa kinanda kwa umahiri mkubwa huku akiongoza Bendi ya Sauti Moja Halisi, kuiba wimbo wa 'Tumepokea Chanzo Halisi' ambao uliufanya ukumbi kuchangamka vya kutosha.Mwimbaji katika Bendi ya Sauti Moja Halisi, akiimba kwa hisia kali, wimbo wa 'Tumepokea Chanzo Halisi' ambao uliufanya ukumbi kuchangamka vya kutosha.Waimbaji katika Bendi ya Sauti Moja Halisi, wakishiriki kuimba kwa wimbo wa 'Tumepokea Chanzo Halisi' ambao uliufanya ukumbi kuchangamka vya kutosha.Mwanamuziki katika Bendi ya Sauti Moja Halisi, akiungurumisha 'domo la bata' kukoleza uhondo wa wimbo wa 'Tumepokea Chanzo Halisi'.
Mwanamuziki wa Bendi hiyo akizicharaza tumba kwa umahiri wa kutosha.
Waimbaji wa Bendi ya Sauti Moja Halisi wakishiriki kuimba wimbo huo.
Mpigagita la solo, akiungurumisha ala hiyo kwa umahiri mkubwa.Wanamuziki wakiimba na kucheza.Wanamuziki wa nyimbo za Sifa za Chanzo Halisi wakishambulia jukwaa kwa kuimba na kucheza.
Mcharaza 'drums' akizicharaza ala hizo kwa kujituma
Baba Halisi akapatwa raha na kupepea kitambaa baada ya kukongwa moyo kwa wimbo wa kumtukuza Chanzo Halisi.
"Katika Mkutano huu, wapo watu mbalimbali hata ambao hawavai vazi jeupe, unajua kuvaa vazi jeupe ni mpaka mtu ajue maana ya vazi hilo, msimlazimishe yeyote kuvaa vazi hilo kama hajajua maana yake. hebu wale wageni wenzetu Waislam ambao huvaa hadi ushungi kama wapo waje hapa mbele niwasalimie, wapewe soda", akasema Baba Halisi.Wale wageni waalikwa wakaanza kuja mbele mmoja baada ya mwingine.
Baadhi yao waliotangulia kufika mbele ya Baba Halisi wakiwa wamesimama kwa upendo Halisi.
Kuhani Moja akawagawia soda."Karibuni sana", Baba Halisi akawaambia wageni hao waalikwa.Wajumbe, Uzao na Makuhani wakiwa ukumbini.
Wajumbe, Uzao na Makuhani baadhi ya waalikwa wakiwa ukumbini.Wajumbe, Uzao na Makuhani wakiwa ukumbini.Wajumbe, Uzao na Makuhani wakiwa ukumbiniKuhani Moja akipokea matunda (Sadaka) maalum.
Wajumbe, Uzao na Makuhani wakiwa ukumbini.Wajumbe, Uzao na wageni waalikwa wakiwa kwenye hema maalum nje ya ukumbi kwa kuwa ndani kulikuwa kumejaa.Wajumbe, Uzao na Makuhani wakiwa ukumbini.
Baba Halisi akaanza kutoa Darasa kuhusu mfumo bora wa kusajili kampuni ya Kiwanda cha Maji cha One Up cha Kanisa Halisi👇
Baba Halisi akiendelea kutoa darasa hilo.
Makuhani walioitwa mbele na Baba Halisi wakiwa na mafaili
Huyu Kuhani akieleza jinsi alivyoelewa Darasa alilotoa Baba Halisi.
Mgeni mwalikwa aitwaye Imani naye akieleza alivyoelewa darasa la Baba Halisi.
Kisha Baba Halisi akamleta mbele Kuhani Moyo Safi na kuwaomba wajumbe wa Mkutano Mkuu huo wampitishe kwa ajili ya kufanya kazi za Utawala, ambapo waliafiki. Sasa atafanya kazi hizo za Utawala na wakati huohuo kuendelea kuwa Mhasibu wa Kanisa hilo.
Baada ya kupitishwa na wajumbe Baba Halisi akampongeza
Ukumbini ikawa furaha kumpongeza Moyo Safi wakati akirejea kuketi. Anayeonyesha furaha hapo mbele ni Kuhani Moja.
Moyo Safi akipongezwa na Kichwa (Mume) wake.Kisha Baba Halisi akamwita Kuhani Bubaberi na kuomba kuwa Katibu wa Makao Makuu ya Kanisa hilo kwa ajili ya kusaidiana na Asteria Mlango ambyae kwa sasa anauguliwa na kichwa (Mume) wake. wajumbe wakaafiki.Baba Halisi akampongeza
Baba Halisi akawaita Vijana wa IT, Kusudi na Utawala wa Amani kuwatambulisha kwa Makuhani na Uzao.
Kisha Baba Halisi akakinadi Kitabu cha Mchango wa Kanisa kwa Taifa kupitia Mikutano ya Kijamii katika mikoa mbalimbali kwa miaka minne (2018-2022). Nakala moja iliuzwa kwa sh. 2000
Kisha Ukawadia wakati wa kupoza koo na tumbo👇
Halafu ukafika wakati wa Kuhani Moja kutoa ripoti ya Kanisa👇
Kuhani Moja akitoa ripoti ya utendaji wa Kanisa Halisi la Mungu Baba katika kipindi cha miaka minne.
Kisha ikafuatia Burudani ya nyimbo za kutukuza Chanzo Halisi👇
Baba Halisi akasitisha Burudani hiyo na kumwita Kuhani Almasi wa Kituo cha Kenya ambaye pia ni Mbunge nchini humo, kwa ajili ya kumtolea mfano wa Uzao wanaounga mkono ujenzi wa Vituo.
"Huyu Kuhani Almasi, aliwahi kuniletea hundi ya fedha nyingi ili kujengwa Kituo, lakini nilikataa, kwa sababu vituo vinapaswa kujengwa kwa michango ya Uzao wote. Lakini hata hivyo ameshabarikiwa", akasema Baba Halisi.
Baba Halisi akimpa nakala ya wimbo mpya wa Bendi ya Sauti Moja Halisi kwa mwimbaji mmoja wa nyimbo za Injili ambaye alialikwa kuhudhuria mkutano huo.
Halafu Kaka Huduma 'akakalia' tena Kinanda kuporomosha Burudani na Bendi hiyo. Ikawa ni Raha mwanzo mwisho ukumbini👇
Baada ya burudani hiyo Baba Halisi akawaita Makuhani kutoka Kenya kwa ajili ya kuombea amani na utulivu uchaguzi mkuu nchini humo.👇
Mama Halisi akipokea shukrani hiyo ya kuombea amani Kenya.
Mama Halisi akimpa Damu safi nyeupe (maji) Baba Halisi ili kupoza koo na kubariki mduara.
Baba Halisi akimnywesha damu safi Kuhani wa Amani Ilala
Kuhani Almasi wa Kituo cha Kenya akizungumza neno la Shukrani.
Baba Halisi akitambulisha baadhi ya Viongozi wakuu wa makao Makuu ya Kanisa Halisi
Akamtambulisha pia kiongozi kutoka Kituo cha Kenya.
Kijana msanii wa kujitegemea wa nyimbo za Injili akitoa neno la shukraniMgeni mwalikwa Imani akitoa neo la Shukrani.
Baba akiondoka kwenye Mduara baada ya kuhitimisha Ibada na Mkutano Mkuu huo.
Kuhani Faida akitangaza utaratibu mwingine kwa wajumbe baada ya Ibada na Mkutano Mkuu huo. Kushoto ni Kuhani Moja.
© May 2022 CCM Blog/Bashir Nkoromo
Shukrani kubwa kwa aliyetuumba
ReplyDelete