Bungeni, Dodoma
Katika hali ambayo haikutarajiwa, Mbunge wa Mbulu Vijijini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Flatei Massay, ameruka sarakasi katika ukumbi wa Bunge, wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa mwaka 2022/2023, Bungeni Jijini Dodoma, leo.
Imeelezwa kwamba Mbunge huyo amefanya tukio hilo kuonyesha msisitizo wa hoja yake kuwa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi imekuwa ikitoa ahadi ya ujenzi wa barabara ya Mbulu hadi Haydom bila utekelezaji.
Flatei amesema licha ya kuahidiwa ujenzi wa barabara hiyo tangu katika bajeti ya mwaka jana, Kamati ya Bunge ya Miundombinu imeonyesha fedha zilizotengwa mwaka jana zimepelekwa kulipa madeni na kwamba katika Kitabu cha Bajeti cha mwaka huu, imeonyeshwa kuwa barabara hiyo itajengwa kwa kiwango cha lami lakini kwa Kilometa 25.
“Kama waliniahidi kuwa barabara itajengwa hilo tangazo linachukua muda gani? Mimi hapa Mheshimiwa Spika sio shilingi tu. Mimi Wananchi wameniambia shilingi niichukue niende nayo Mbulu Vijijini maana hapa hamna namna tena,” Flatei akasema.
Kisha akamwambia Spika wa Bunge Dk. Tulia Ackson akisema kwamba kama hamtoi ndani ya ukumbi wa Bunge basi apige sarakasi humo humo.
“Mimi naona wanataka kunitengenezea ajali kuliko kukitengenezea ajali chama changu si bora uruhusu tu niruke hapa ili wastuke sasa nitafanyaje sasa,” akasema.
Akasema licha ya kusema kwenye bajeti mwaka jana ameuliza maswali saba mwaka jana na manne mwaka huu.
“Mheshimiwa spika nisaidie ninafanyaje? Nimezungumza nao sana, sasa inatosha na kwasababu sitaki kuruka hapa. Mipango yote nimefuata utaratibu wote nimefuata inatia uchungu mheshiwa Spika,”akasema.
Your Ad Spot
May 23, 2022
MBUNGE WA MBULU VIJIJINI ARUKA SARAKASI BUNGENI KUDAI BARABARA
Tags
featured#
siasa#
Share This
About Bashir Nkoromo
siasa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇