LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 26, 2022

KATIBU WA CCM WILAYA YA KIGAMBONI MKANDAWILE ARIPOTI OFISINI, APOKEWA KWA SHANGWE, AWATAKA VIJANA KUTANGAZA UTENDAJI WA RAIS SAMIA

Na Bashir Nkoromo, Kigamboni
Katibu mpya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kigamboni, Dar es Salaam Stanley Mkandawile amewataka Vijana  wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) kuwa mstari wa mbele kusema kwa wananchi yote aliyokwishafanya na anayofanya Rais Samia Suluhu Hassan katika kuliletea Taifa maendeleo ya kiuchumi na Kijamii katika nyanja mbalimbali.

Mkandawile amesema, ni wajibu wa Vijana hao kuyasema hayo kwa kuwa wengi wao ni wasomi na wanao uwezo wa kuyafafanua vema kwa wananchi ili yapate kujulikana kwa kuwa kuna baadhi ya watu wamekuwa wakisema Rais Samia hajafanya lolote katika kuleta maendeleo ya Kiuchumi wala ya Kijamii tangu aingie madarakani, sababu kubwa ikiwa ni kwakuwa mengi yaliyofanyika hawayajui.

Aliyasema hayo jana, alipokuwa akizungumza na Vijana wa UVCCM  Vyuo na Vyuo Vikuu Seneti ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na baadhi ya vyuo vilivyopo katika Wilaya ya Kigamboni, alipofika kwenye Kikao chao cha kukumbushana masuala ya hamasa kilichokuwa kinafanyika Ofisi ya CCM wilayani hapo.

Mkandawile alifika kwenye kikao cha Vijana hao kwa lengo la kuwasalimia, baada ya kuripoti rasmi katika Ofisi ya CCM Wilaya hiyo ya Kigamboni kwa mara ya kwanza tangu apewe barua ya uhamisho na Makao Makuu ya CCM kuwa Katibu wa CCM wa Wilaya hiyo kuchukua nafasi iliyoachwa wazi  na David Mollel ambaye amekuwa Katibu wa CCM mkoa wa Ruvuma.

"Tunajua kuwa zipo chanagamoto mbalimbali zinazotukabili Watanzania, lakini ninyi vijana wa CCM ni lazima muwe wa kwanza kutambua kuwa pamoja na changamoto hizo lakini yapo mambo makubwa ambayo Rais Samia ameyafanya na anaendelea kuyafanya ili kuhakikisha Taifa hili la Tanzania linainuka zaidi kiuchumi na kijamii.

Hivyo ni wajibu wenu kama vijana wa CCM myaseme kwa wananchi yale aliyokwishafanya na anayoendelea kuyafanya, badala na ninyi kujiunga na walalamikaji ambao wengi wao wanafanya hivyo kwa sababu hawayajui aliyofanya na anayoendelea kuyafanya Rais wetu", alisema Mkandawile.

"Bila shaka mnayajua mambo ambayo Rais Samia ameyafanya hasa katika kipindi chake cha mwaka mmoja tangu ashike uongozi. Haya ndiyo mnatakiwa kuwaambia wananchi wasioyajua. Kwa mfano, Rais Samia amepunguza gharama za matibabu ya figo kwa asilimia 66, Katika miezi sita ya kwanza ya Rais Samia uwekezaji ulikua kwa asilimia 400, ukafikia Dola Bilioni 3 kutoka Dola za Marekani Milioni 510.

Waambieni wananchi, Rais Samia ameweka historia katika kubiresha Sekta ya Elimu, kwa kujenga madarasa mapya manne ( 4 ) katika kila ilipo shule ya Sekondari ya Serikali nchi nzima na kuvunja rekodi ya kuwezesha Watoto wote zaidi ya milioni moja  wa kidato cha kwanza nchi nzima kuanza shule siku moja." akasema Mkandawile na kuongeza;

"Bila shaka ninyi (aliokuwa akizungumza nao) ni wasomi mpo vyuoni mnajua kuwa Rais Samia ameongeza fedha za Mikopo ya Elimu ya Juu kutoka Sh. Bilion 464 hadi kufikia Sh. Bilion 570 inayonufaisha Wanafunzi zaidi ya 160,000, sasa mambo kama haya mkisaidia kuwaambia wananchi wakayajua mtakuwa mmekisaidia sana Chama Cha Mapindizi".

"Nilikuwa Katibu wa CCM Wilaya ya Kibondo, huko kulikuwa na adha kuwa wanayopata wakulima. ilikuwa ikifika mwezi Januari, wananchi wanashindwa kwenda mashambani, wanaenda mafichoni kuhofia kukamatwa kwa ajili ya kwenda kujenga madarasa.

Sasa Rais Samia amewakomboa, maana badala ya kujenga wao madarasa kila ifikapo Januari, sasa amejenga mwenyewe madarasa ya kutosha." akasema Mkandawile na kuongeza;

 "Hebu fikirieni yaani Rais amejenga madarasa 15,000 nchi nzima, amevifungulia vyombo vya habari vilivyokuwa vimefungiwa, juzi juzi amepandisha mishahara kwa Wafanyakazi kwa asilimia 23.3, amefuta stakabadhi ghalani kwa mazao ya Pamba, dengu Choroko, Mbaazi na Ufuta", sasa mambo kama haya mkijituma mkawaambia wananchi hawatamwelewa kweli Rais wetu Mama Samia?".

Mapema kabala ya kuzungumza na Vijana hao wa UVCCM, Mkandawile baada ya kuwasili Ofisi ya CCM Wilaya ya Kigamboni alipokewa kwa bashasha na Viongozi waliokuwepo ofisini hapo na baada ya kusaini vitambu vya wageni japo wanamjua alijitambulisha na kukabidhi barua yake ya kuteuliwa kuendelea na Ukatibu wa Wilaya katika wilaya hiyo.

"Kwa kweli nakishukuru Chama Cha Mapinduzi kunileta wilaya hii, ni wilaya wenye wana CCM wachapakazi, lakini naomba niseme tu kwamba mimi hapa sikuletwa kuwa 'bosi' nimeletwa kuja kufanya kazi kuwa kiongozi ninayetangulia mbele siyo kiongozi anayebaki nyuma na kutoa maelekezo tu. kwa ufupi ni kwamba tutafanya kazi kwa pamoja.

Naomba mjue ndugu zangu, ili tufanye kazi kwa ufanisi lazima tutambue kwamba watumishi wa Chama wa ngazi zote tunategemeana maana tusipotegemeana kazi haitaenda vizuri kama anavyotutarajia mwajiri wetu", akasema Mkandawile.

Katibu mpya wa CCM Wilaya ya Kigamboni, Dar es Salaam akikabidhi barua yake kwa aliyekuwa Kaimu Katibu wa CCM Wilaya hiyo, Katibu wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Kigamboni Catherine Mwenda, alipofika kuripoti rasmi jana. Wwengine kutoka watatu kushoto ni Katibu Mwenezi Kigamboni Abdallah Pazi Shomari, Katibu wa UVCCM Kigamboni Ashura Kizigo, Lucy Masota afisa katika Ofisi hiyo ya CCM Wilaya ya Kigamboni na Mhasibu wa Ofisi hiyo Francis Lumeta.

Mwanzo: Mkandawile alipowasili Ofisi ya CCM Kigamboni👇

Mkandawile akipokewa na Mhasibu wa CCM Wilaya ya Kigamboni Francisi Lumeta.
Mkandawile akiingia kwenye jengo la ofisi ya CCM Kigamboni
Mkandawile akilakiwa na Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Kigamboni Caterine Mwenda baada ya kuwasili katika ofisi yake. Catherine alikuwa Kaimu Katibu wa CCM Wilaya hiyo ya Kigamboni.
Mkandawile akisalimiana kwa furaha na Katibu Mwenezi wa Kigamboni Abdallah Pazi.
Mkandawile akisaini vitabu vya wageni. Kulia ni Catherine Mwenda.
Mkandawile akiendelea kusaini vitabu vya wageni.
"Huyu ndiye alikuwa anakaimu nafsi uliyokuja kushika "Katibu Mwenezi Pazi akimtambulisha Chatherine kwa Mkandawile.
Kisha katibu Mwenezi akazungumza machache kumkaribisha Mkandawile. Mkandawile akacheka kwa furaha.
Kisha wakacheka wote kwa furaha.
Mkandawile akikabidhi barua yake kwa aliyekuwa akikaimu nafasi ya katibu wa CCM Wilaya ya Kigamboni huku baadhi ya viongozi wakshuhudia.
Mkandawile akisalimiana na Mhasibu wa CCM Wilaya ya Kigamboni Francis Lumeta.
Kisha akamsalimia Lucy Masota afisa katika Ofisi hiyo ya CCM Wilaya ya Kigamboni.
"Hapa sikuja kuwa bosi, nimekuja kuwa mfanyakazi mwenzenu', akasema Mkandawile baada ya kukabidhi barua yake.
Mkandawile akizungumza na Vijana wa Hamasa wa UVCCM kutoka Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kivukoni na vyuo vingine vya Wilayni Kigamboni ambao alipita kuwasamia wakiwa kwenye kikao  cha kukumbushana makujumu.
Vijana hao wakimsikiliza kwa utulivu wa kutosha.
Katibu wa UVCCM Wilaya ya Kigamboni ashura Kizigo akizungumza.
Mkandawile akiwa na Vijana hao katika picha ya pamoja.
Mkandawile akisindikzwa na katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Kigamboni Abdallah Pazi wakati akitoka. Anayewafuata ni Katibu wa UVCCM Wilaya ya Kigamboni Mponela Mathei.
Mkandawile akiwa na Vijana hao katika picha ya pamoja nje ya jengo la Ofisi ya CCM Wilaya ya Kigamboni.

Mkandawile akiwa na Vijana hao katika picha ya pamoja nje ya jengo la Ofisi ya CCM Wilaya ya Kigamboni.
Mkandawile akimsikiliza katibu Mwenezi wa Wilaya ya Kigamboni Abdallah Pazi wakati wanaagana kabla hajaondoka.
Mkandawile akiwapiga vijana hao msasa wa mwisho mwisho kabla ya kuondoka.
Kisha akaagana na Katibu Pazi maneno ya mwisho mwisho kabla ya kuondoka.

Mkandawile akimalizia kwa kupigapicha ya kumbukumbu na Kijana wa UVCCM Elisha wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni.

 © May 2022 CCM Blog/Bashir Nkoromo


 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages