LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 20, 2022

GENZABUKE AMPONGEZA WAZIRI MKUU MAJALIWA KUHAMASISHA KILIMO CHA MICHIKICHI KOGOMA+video

 Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Kigoma, Josephine Genzabuke, amempongeza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwa kuhamasisha kilimo cha Michikichi mkoani Kigoma.

Aidha, Genzabuke amemshukuru Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe kwa kumpatia miche 3000 ya michikichi na kuomba amuongeze mingine ili aendelee kuisambaza kwa wakulima na hasa wanawake mkoani humo. Ametoa pongezi na shukrani hizo alipokuwa akichangia mjadala wa makadirio ya Bajeti ya Kilimo bungeni Dodoma Mei 18, 2022.

Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Genzabuke akitoa mchango wake huo...
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA 
 MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM 
 0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages