LENGO KUU
Fedha za Mfuko wa Jimbo zitatumika kuchangia ujenzi na uboreshaji wa baadhi ya miundombinu kwenye Sekondari za Kata. Miundombinu itakayochangiwa ni:
*Ukamilishaji wa Maabara
*Ukamilishaji wa Maktaba
*Ujenzi wa Mabweni
SEKONDARI ZILIZOTUMA MAOMBI
A - Sekondari zilizotuma maombi ndani ya muda uliowekwa
1. Kigera 2. Kiriba
3. Mkirira 4. Seka
5. Nyakatende
6. Makojo
7. Nyasaungu (mpya, inajengwa)
B - Sekondari zilizochelewa kutuma maombi:
8. Murangi 9. Tegeruka
10. Mugango 11. Bulinga
UTARATIBU UNAOTUMIKA
1. Makisio ya Vifaa vya ujenzi vitakavyonunuliwa kutokana na Fedha za Mfuko wa Jimbo zilizotolewa. Tunazo Tshs 52.4m
2. Kikao cha Kamati ya Mfuko wa Jimbo kujadili na kugawa vifaa vya ujenzi. Mwenyekiti wa Kikao ni Mbunge wa Jimbo
3. Halmashauri yetu ndiyo inanunua vifaa vya ujenzi kwa kutumia Fedha za Mfuko wa Jimbo
4. Wapokeaji wa vifaa vya ujenzi wanagharamia usafirishaji wa vifaa walivyogawiwa
KIKAO CHA KUGAWA VIFAA VYA UJENZI
Mahali
*Kijijini Nyang'oma, Mugango
*Ofisi za Halmashauri yetu
Siku na Muda
Jumatatu, 16.5.2022
Saa 4 Asubuhi
WATAKAOHUDHURIA
*Wajumbe wa Kamati ya Mfuko wa Jimbo
*Waliotuma maombi
*Wananchi wanakaribishwa, hiki ni kikao cha wazi
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇