CCM HQ, Dodoma
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imeunga mkono na kuridhia hatua ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan, kuendeleza majadiliano na vyama vya siasa yenye lengo la kuimarisha Demokrasia kupitia maridhiano ya kisiasa kwa maslahi ya Taifa.
Pia Kamati Kuu imesisitiza CCM kuendeleza majadiliano hayo kwa dhumuni la kujenga jamii yenye usawa, uhuru wa kujieleza na kushiriki shughuli za kisiasa kwa kuzingatia maadili na sheria za nchi.
Hayo yamesemwa leo na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka, wakati akizungumza katika Makao Makuu ya CCM Jijini Dodoma, na kufafanua kuwa Kamati Kuu hiyo iliyofanya kikao chake juzi chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais Samia, ilipokea na kujadili masuala mbalimbali ya Kitaifa, ikiwemo hatua zinazochukuliwa na Rais Samia katika kujenga maridhiano ya kisiasa nchini.
Shaka amesema Kamati Kuu imetambua na kuridhia dhamira ya dhati ya Rais Samia ya kufanya maridhiano kwa kuzingatia uendelezaji wa urithi, tunu na msingi imara wa ujenzi wa taifa iliyoachwa na Waasisi wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere na Hayati Abeid Amani Karume, ili kuviwezesha vizazi vijavyo virithi taifa jema na lililo imara.
Shaka amesema CCM inatambua mazingira na mahitaji ya kisiasa yaliyopo ndani ya jamii kwa sasa, hivyo kufanikiwa kwa majadiliano hayo kutawanufaisha wananchi katika kuimarisha misingi ya utawala bora na utoaji huduma za kijamii.
“CCM ndicho chama kiongozi na kikomavu katika siasa za nchi yetu, kipo tayari kuendeleza mjadala wenye lengo la kuimarisha demokrasia endelevu kwa maslahi ya Taifa,” alisisitiza Shaka na kutoa rai kwa Watanzania kuendelea kumuunga mkono Rais Samia kwa kuwa amekuwa kiongozi mwenye kuliunganisha Taifa.
Your Ad Spot
May 23, 2022
Home
featured
Kitaifa
CCM YAMUUNGA MKONO RAIS SAMIA KWA KUENDELEZA MAJADILIANO NA VYAMA VYA SIASA KUIMARISHA DEMOKRASIA KUPITIA MARIDHIANO
CCM YAMUUNGA MKONO RAIS SAMIA KWA KUENDELEZA MAJADILIANO NA VYAMA VYA SIASA KUIMARISHA DEMOKRASIA KUPITIA MARIDHIANO
Tags
featured#
Kitaifa#
Share This
About Bashir Nkoromo
Kitaifa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇