Akizungumza leo jijini Arusha Mkuu wa Mkoa Arusha John Mongella amewaomba wananchi kujitokeza saa 12:00 asubuhi kumpokea Rais samia Hassan Suluhu atakayekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo.
Pia ameomba viongozi wote watakaoshiriki uzinduzi huo amewaomba wafike saa 5:00 asubuhi Hoteli ya kitalii Mount Meru kuegesha magari yao na kupanda usafiri wa pamoja aina ya Coaster iliyoandaliwa na serikali kwaajili ya kuwapeleka ukumbi wa AICC.Amesema kuwa, AICC hataruhusiwa mtu yoyote kuingia na gari lake binafsi, ili kuweka utulivu kwa ajili ya uzinduzi huo.
“Hapa tunaweka utaratibu huu ili wawahi ukumbini na wote wawe wamefika eneo la tukio saa nane kamili mchana kwa sababu Rais Samia akishaingia ukumbini hataruhusiwa mtu kuingia AICC,”amesema.
Aidha amesema kuwa, barabara ya Goliondoi na Azimio la Arusha hadi mnara wa saa itafungwa kwa ajili ya kuruhusu wananchi kutembea bila wasiwasi kuelekea AICC.
Mongella amesema kuwa,wananchi watakaojitokeza kushuhudia uzinduzi huo AICC wameandaliwa eneo maalum la kukaa lenye uwezo wa kubeba watu zaidi ya 6000.
“hapa nawaomba wananchi mjitokeze kushuhudia tukio hilo, ambalo tunaandika historia ya nchi yetu na kila mtu atapata pa kukaa bila shida, wala msiogope kuja ni tukio la kila mwananchi bila ubaguzi wa aina yoyote,”amesema.
Amesema kuwa, kila atakapokaa mwananchi kumeandaliwa luninga za kuangalia uzinduzi huo bila kukosa.
Ameomba pia sekta binafsi kujiandaa vema kwenye kampuni zao kwa ajili ya kupokea wageni kwani baada ya uzinduzi huo wanatarajia kupokea watalii wengi.
Mongella amesema Rais amefungua milango na kinachotakiwa sekta binafsi kujipanga katika kuimarisha huduma zao.
Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Justine Masejo, amesema jeshi la Polisi limejiimarisha ili kuhakikisha usalama unakuwepo zaidi ya siku zote.
“Hapa nawaomba wananchi wasiwe na wasiwasi watakapoona ulinzi umeimarishwa kila eneo, sababu tukio hili kubwa na tunashirikiana na wenzetu na tayari vikosi vya ulinzi vya mikoa jirani vimeshawasili mkoani hapa kuongeza nguvu ya ulinzi,”amesema.
Filamu hiyo ilizinduliwa Aprili 18 New York ,Aprili 21 mwaka huu, Los Angeles nchini Marekani na Aprili 28 mkoani Arusha,kisha Mei 7, Zanziba na Mei 8 Dar es Salaam.
Waandaaji wa Filamu hiyo Peter Greenberg na Timu yake ya Royal Tour na ilirushwa na vituo vya Televisheni 350 na wameweka kwenye Applications za Amazon Prime na Apple TV Plus ikiwa na lengo la kutangaza na kuifungua nchi kwa ajili ya kuwezesha upatikanaji wa watalii na wawekezaji ili kukuza uchumi wa nchi.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇