Urusi na Marekani leo zimetangaza kubadilishana wafungwa licha ya mivutano mikali inayoshuhudiwa baina ya madola hayo mawili yenye nguvu za kijeshi kuhusiana na vita nchini Ukraine.
Moscow imemwachia mwanajeshi wa zamani wa Marekani Trevor Reed aliyefungwa nchini Urusi mwaka 2020 huku Washington ikitangaza kumwachia rubani wa kirusi aliyehukumiwa kifungo cha miaka 20 kwa makosa ya kusafirisha dawa za kulevya.
Rais Joe Biden wa Marekani amesema ilikuwa jambo gumu kufikia uamuzi huo lakini hiyo ni ishara kuwa utawala wake unatoa kipaumbele katika kuwarejesha nyumbani wamarekani wanaoshikiliwa kimakosa ughaibuni.
Urusi nayo imesema tukio hilo la kubadilishana wafungwa ambalo halikutarajiwa ni matokeo ya mchakato mrefu wa mashauriano baina ya mataifa hayo mawili.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇