Uturuki imekuwa ikivuka mpaka na kuendesha operesheni kadhaa dhidi ya PKK katika miongo kadhaa iliyopita.
Na mashambulizi ya hivi karibuni yalijikita zaidi katika maeneo ya kaskazini mwa Iraq ya Metina, Zap na mikoa ya Avashin-Basyan.
Wiki iliyopita, Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alikutana na Masrour Barzani, waziri mkuu wa eneo linalojitawala la Wakurdi ambalo linadhibiti maeneo yaliyoshambuliwa.
Waziri wa Ulinzi wa Uturuki amesema uvamizi huo ulilenga magaidi na kwamba walijaribu kuepuka maafa kwa raia na uharibifu wa miundo ya kitamaduni na kidini.
Hakukuwepo taarifa kutoka kwa kundi la wanamgambo hao wa Kikurdi juu la shambulio hilo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇