Kenya na Zimbabwe zitajumuishwa katika droo ya kufuzu kwa mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2023 kesho Jumanne mjini Johannesburg, Afrika Kusini licha ya kupigwa marufuku na shirikisho la soka duniani FIFA kutokana na uingiliaji wa serikali katika masuala ya soka.
Msemaji wa Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF), amesema wamezijumuisha nchi hizo mbili kwa matumaini kwamba marufuku itaondolewa wiki mbili kabla ya siku ya kwanza ya mechi za mwezi Juni.
Shirikisho la michezo la Zimbabwe liliibua hasira ya FIFA kwa kuwatimua watendaji wa chama cha soka cha kitaifa huku maafisa wa wizara ya michezo ya Kenya wakilivunja shirikisho la soka la kitaifa baada ya rais wake, Nick Mwendwa, kushtakiwa kwa makosa kadhaa ya ulaghai.
CAF imeweka muda wa mwisho wa katikati ya Mwezi Mei na iwapo marufuku hiyo itakuwa haijaondolewa, nchi hizo zitazuiwa kushiriki.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇