Naibu Waziri wa Afya Dkt Godwin Mollel akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchangiaji damu katika Chuo Kikuu cha Afya Shirikirishi Muhimbili kuelekea wiki ya maandalizi ya kongamano kubwa litakalofanyika hivi karibuni
kuzungumzia Saratani yaDamu ambayo inapunguza kiasi cha Damu mwilini.
Tupo katika zoezi la kuzunguuka Kanda zote za Nchi yetu kuhakikisha swala la upatikanaji wa Damu salama na linakuawa si tatizo tena na nikiwapongeza Wanavyuo, Wanafunzi na wananchi kwa ujumla kwa kuitikia na kuwa na hamasa ya kujitokeza kuchangia Damu.
Pia na kuwaomba Watanzania tuendelee kujitokeza kwani damu haiuzwi na tukumbuke kuwa tunawapoteza mama wengi na pia tunapoteza watu wetu kwa ajali aliendelea kusema Mollel huku akiwaomba Wananchi kuendelea kuona umuhimu wa kujitolea kuchangia Damu na iwe historia.
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Dkt. Omary Ubuguyu akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchangiaji damu Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).
Meneja wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama Dkt. Magdalena Lyimo akisema jambo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchangiaji damu Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).
Afisa Uhusiano wa MUHAS, Hellen Mtui akitoa akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchangiaji damu katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).
Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Aifello Sichalwe akizungumza jambo leo Aprili 4, 2022 wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchangiaji damu katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).
Afisa Viwango na Ubora Kanda ya Mashariki Mpango wa Taifa wa Damu Salama. Sam Mduma (kushoto) akizungumza na Madaktari Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Prof. Appolinary Kamuhabwa (kushoto) akimsikiliza Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchangiaji damu katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) leo Aprili 4, 2022.
No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇