Na Bashir Nkoromo, CCM Blog
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)- Bara kanamli Mstaafu Abdulrahman Kinana amepokelewa kwa kishindo baada ya kuwasili mkoani Tanga, akiwa katika siku yake ya pili ya ziara yake ya kwanza kuifanya mikoani kukagua na kuimarisha uhai wa Chama na utekelezaji wa Ilani ya CCM tangu achaguliwe na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM mwanzoni kabisa mwa mwezi huu, Jijini Dodoma.
Katika ziara hiyo ambayo aliianza jana katika mkoa wa Pwani, Kinana ambaye ameambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya taifa (NEC), Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka, baada ya kuwasili leo mkoani Tanga, amepokewa na mamia ya wanachama wa CCM, wakiongozwa na viongozi wa ngazi mbalimbali wakiwemo Wabunge na Mwenyekiti wa CCM mkoa huo Henry Shekifu.
Kabla ya kufanyika mkutano Wilayani Korogwe ambapo mapokezi yake maalum yamefanyika, Kinana alikutana na Viongozi na kupewa taarifa ya maendeleo, uhai wa Chama na Itekelezaji wa Ilani ya Chama ya mkoa wa Tanga.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti viongozi wa CCM Mkoa wa Tanga wakiongozwa na Shekifu, wamesema pamoja na mafanikio Utekelezaji wa Ilani ya Chama, utekelezaji huo unaendelea kufanyika ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wa mkoa huo na kwamba utekelezaji unakwenda vizuri kutokana na usimamizi mzuri unaofanywa na Chama.
Kwa jumla Viongozi wa mkoa huo wa Tanga wamemuahidi Kinana kwamba watahakikisha mkoa wao Kichama unakuwa mkoa ambao hautakuwa tegemezi kwa kuwa tayari wameshaweka mipango thabiti ya kuhakikisha unakuwa mkoa ambao unajitegemea kiuchumi.
Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga Suleiman Mzee Suleiman amemwambia Kinana kuwa mkoa huo unampongeza kwa kuteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM- Bara na anastahili kupewa heshima hiyo kutokana na uzalendo wake uliotukuka kwa Taifa la Tanzania.
Akitoa salam kwa niaba ya Mkuu wa mkoa huo Adam Malima, Katibu Tawala Mkoa wa Tanga amesema kwamba wanaendelea kuchapaka kazi ili kuleta maendeleo katika nyanja mbalimbali.
Pamoja na mambo mengine amewasilisha taarifa ya Mkoa wa Tanga iliyokuwa inaelezea masuala mbalimbali huku akizungumzia mchakato wa Anuani za Makazi ambao alisema umefanyika kwa mafanikio makubwa kwa kutambua mchakato huo wa anuani za makazi utakwenda kusaidia katika sense ya watu na makazi inayokwenda kufanyika Agosti mwaka huu.
Pia ametoa taarifa ya ujenzi wa makazi ya wananchi ambao wamehamishiwa Wilaya ya Handeni katika Mkoa wa Tanga wakitokea Hifadhi ya Ngorongoro na kwamba ujenzi wa makazi kwa ajili ya wananchi hao unakwenda vizuri na mkoa umetenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa shule.
Baada ya ziara ya mkoa wa Tanga kesho Kinana anatarajiwa kuendelea na ziara yake mkoani Kilimanjaro ambako pia itarajiwa kuwa atapata mapokezi makubwa kama mkoa huo wa Tanga na mkoa wa Pwani.
Imehaririwa kutoka Michuzi Blog
Habari kwa Picha
Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana akiwasili katika ukumbi Mjini Korogwe, kuanza ziara katika mkoa huo, leo.Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana akivishwa skafu baada ya kuwasili Korogwe kuanza ziara yake katika mkoa wa Tanga, leo. Kushoto ni Mwenyeji wake, Mwenyekiti wa CCM mkoa huo Henry Shekifu.Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana akifurahia brudani ya ngoma iliyochezwa kumpokea, baada ya kuwasili Korogwe kuanza ziara yake katika mkoa wa Tanga, leo.Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Viongozi mbalimbali baada ya kuwasili Korogwe kuanza ziara yake katika mkoa wa Tanga, leo. Pamoja naye ni Mwenyekiti wa CCM mkoa huo Henry Shekifu.Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana akifurahi na kinamama wa CCM waliokuwa kwenye mapokezi, baada ya kuwasili Korogwe kuanza ziara yake katika mkoa wa Tanga, leo.Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana akitazama kitabu chenye picha ya Mwenyekiti wa CCM Rais samia Suluhu Hassan ambacho kilimvutia baada ya kukiona kwa mwana CCM Mjasiriamali aliyekuwa anauza nje ya ukumbi, vitu mbalimbali vinavyohusu CCM, baada ya kuwasili Korogwe kuanza ziara yake katika mkoa wa Tanga, leo.Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Viongozi mbalimbali baada ya kufika eneo la Mkutano, baada ya kuwasili Korogwe kuanza ziara yake katika mkoa wa Tanga, leo. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa huo Henry Shekifu.Wana CCM na Viongozi mbalimbali wakiwa wamesimama huku wakiimba kumlaki Kinana ukumbini.Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana akiwa amesimama kusalimia wana CCM na Viongozi mbalimbali baada ya kuwasili ukumbini.Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana na Viongozi wenzake Meza Kuu wakiungana na wana CCM na Viongozi mbalimbali ukumbini.Baadhi ya Viongozi wakiwemo Wabunge kutoka mkoa wa Tanga Kama Januari Makamba na Mwana FA, wakijumuika kushangilia baada ya Kinana kuwasili ukumbini.Ukumbi ukiwa umefurika wana CCM kumsikiliza Kinana.Baadhi ya wana CCM waliokosa nafasi ndani ya ukumbi wakiwa kwenye eneo maalum nje ili mradi kumsikiliza Kinana.Picha zote kwa Hisani ya Michuzi Blog/Tv
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇