Ikungi, Singida
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Jerry Murro amesema Tanzania Bara haiwezi kuwa salama kama Zanzibar haitakuwa salama kiulinzi, kiuchumi na kijamii.
Amesema wakati dunia ikiungana katika muktadha mbalimbali ni vizuri kwa Tanzania kudumisha Muungano wao ili kutoa nguvu ya kuleta maendeleo kwa jamii za pande zote mbili za Muungano huo.
Muro ameyasema hayo wakati akifungua Kongamano la Vijana mkoa wa Singida, ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya miaka 58 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo alifungua kongamano hilo kwa niaba ya Mkuu wa mkoa huo Dk. Binilith Mahenge.
Kongamano hilo limefanyika katika ukumbi wa mikutano ya chuo cha uhasibu Singida ambapo mada mbalimbali zimejadiliwa ikiwemo umuhimu wa kudumisha muungano, fursa za uchumi katika mkoa wa singida na ushiriki wa vijana katika sensa ya watu na makazi.
Your Ad Spot
Apr 26, 2022
Home
featured
siasa
DC IKUNGI : TANZANAIA BARA HAIWEZI KUWA SALAMA KAMA ZANZIBAR HAITAKUWA SALAMA, KIUCHUMI, KIJAMII.
DC IKUNGI : TANZANAIA BARA HAIWEZI KUWA SALAMA KAMA ZANZIBAR HAITAKUWA SALAMA, KIUCHUMI, KIJAMII.
Tags
featured#
siasa#
Share This
About Bashir Nkoromo
siasa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇