*Ampongeza Rais Samia kwa kuwezesha hatifungani kutolewa.
*Asisitiza Uwekezaji uwe wenye tija na endelevu,
*Bodi yaahidi
kutekeleza majukuumu kwa uadilifu.
Na Mwandishi Wetu, Arusha
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemav, Profesa
Joyce Ndalichako amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa
Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha kutolewa kwa hatifungani kama malipo ya deni
la Serikali kwa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF).
Profesa Ndalichako alisema hayo Ijumaa, Machi 11, 2022
jijini Arusha alipokuwa akizindua Bodi ya Wafadhamini ya PSSSF iliyoteuliwa Disemba
mwaka jana.
“Tunamshuru sana Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan
ndani ya kipindi cha mwaka mmoja amewezesha kutoa trilioni 2.17 kwa ajili ya
kulipa deni hilo lililodumu kwa muda mrefu.
Akizungumzia kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Bodi
aliyoizindua, Mhe. Ndalichako alisema; “Natoa rai kwa Bodi kuhakikisha
mnatekeleza majukumu yote. Nawapongeza kwa sababu Mfuko umeendelea kukua,
naomba mhakikishe maswala yote ya fedha mnayasimamia vizuri ili tuweze kulipa
mafao. Naomba mhakikishe mnawekeza kwenye miradi yenye tija”.
Akizumgumzia uwekezaji, Mheshimiwa Waziri alielekeza
uwekezaji uwe kwenye miradi yenye tija na endelevu na Mfuko uendelee kumuunga
mkono Mheshimiwa Rais kwa kuwekeza kwenye viwanda vyenye uhakika wa kuongeza
ajira na vinavyotumia malighafi zinazopatikana nchini.
“Nafahamu mnawekeza katika viwanda, mfano kiwanda cha Karanga (kiwanda cha bidhaa za ngozi cha Kilimanjaro), jana nilivaa viatu vya Karanga, ni vizuri sana, nawapongeza sana. Kiwanda hiki kitasaidia sana wafugaji wetu kuuza ngozi” alifafanua.
Kwa upande wa watumishi wa PSSSF, Mheshimiwa Waziri
aliwataka kufanya kazi kwa pamoja na ushirikiano ili kufikia malengo
yaliyopangwa.
Akizungumza
katika hafla hiyo Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba alimpongeza,
Mheshimiwa Prof. Joyce Ndalichako kwa kuteuliwa na Rais, Samia Suluhu Hassan
kuwa Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu
Akizungumzia
utendaji wa Mfuko CPA Kashimba alisema tangu kuanzishwa kwake, Mfuko
unatekeleza majukumu yake vyema chini ya usamimazi wa Bodi ya Wadhamini na
kuongeza kuwa changamoto zilizokuwa katika mifuko iliyounganishwa zimefanyiwa
kazi na sasa wanachama wa PSSSF wanapata huduma bora kwa kiasi kikubwa.
Wajumbe
wa Bodi ya Wadhamini iliyozinduliwa inajumuisha; Mhandisi Musa Iyombe ambaye ni
Mwenyekiti, pamoja na wajumbe wengine ambao ni; Dkt. Aggrey K. Mlimuka, Bi. Suzan
B. Kabogo, CPA Stella E. Katende, Bw. Victor F. Kategere, Bi. Mazoea Mwera, Bw. Thomas C. Manjati, Bw. Said A.
Nzori na Bw. Rashid M. Mtima. Bodi ya Wadhamini ya PSSSF imeundwa kwa
kuzingatia utatu wa uwakilishi kutoka Serikalini, Wafanyakazi na Waajiri.
Akizungumza
baada ya uzinduzi wa bodi, Mwenyekiti wa Bodi hiyo Mhandisi Musa Iyombe
alisema, “Tunashukuru sana Mhe. Waziri kwa kuja kutufungulia, asante sana.
Nakuhakikishia kazi ya Bodi ni kukushauri na maagizo yako yote sisi kama Bodi
tutatekeleza pamoja na majukumu yetu kwa uaminifu na uadilifu, tupo makini
hatutakuangusha.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe. Profesa. Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya PSSSF mara baada ya kuizindua rasmi leo jijini Arusha.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇