Na Bashir Nkoromo, CCM Blog, Mabibo
Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wametakiwa kutumia fursa ya Mitandao ya Kijamii kuijenga CCM na kujitafutia fursa za kujielimisha zinazopatikana katika mitandao hiyo, badala ya kuitumia kupiga soga na kufanyia mambo mengine yasiyo na manufaa katika maisha yao ya sasa na ya baadaye.
Wamefundwa kuwa ikiwa Vijana hao hasa wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wakiitumia vilivyo mitandao ya kijamii wataiinua CCM katika mambo kadhaa ikiwemo kutangaza Itikadi na Ilani ya Chama na kazi mbali mbali zinazofanywa na Serikali katika kutekeleza Ilani, ili yote hayo yajulikani kwa wananchi wengi.
Hayo yamesemwa leo na Afisa Tehama wa Makao Makuu ya CCM Levina Myovela na Mhazili Msaidizi wa Chuo hicho cha NIT Jamila Mkomwa wakati wakizungumza kwa nyakati tofauti katika Kongamano la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Tawi la NIT, Mabibo Jijini Dar es Salaam, lililofanyika katika Chuo hicho.
"Kuna mambo mengi ambayo ninyi Vijana mnaweza kuyafanya na yakakiinua Chama Cha Mapinduzi, kama kutangaza ilani ya CCM na pia kuzitangaza shughuli zinazofanywa na Viongozi wetu wa Chama na zinazofanywa na Serikali ya CCM katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi, haya mkiyatangaza vya kutosha wananchi wengi wakayajua CCM itaneemeka", alisema Levina.
Akizungumzia mitandao hiyo ya Kijamii, Mhazili Msaidizi wa Chuo hicho cha NIT Jamila Mkomwa naye alisema, inashangaza sana kuona Vijana wanaosoma katika chuo hicho na kwingineko wanatumia mitandao ya Kijamii kama facebook, Instagram na WhatsApp kubadilishana mawazo ya hovyo badala ya kuitumia kujiimarisha kimasomo na kujipatia maarifa.
"Tazama, hapa NIT kuna internet ya bure kupitia WiFi inayogharamiwa na Chuo, lakini ninyi vijana mnaosoma hapa hamuitumii kujipatia manufaa ya kimasomo na fursa zingine zikiwemo hata za kibiashara na za kujipatia nafasi za masomo hadi nchi za nje", alisema Jamila.
Aliwaasa Vijana hao kwamba wakati wanasoma wakitafakari pia kuhusu maisha yao ya baadaye, na siyo kujisahau wakidhani maisha ya kuhudumiwa na wazazi na kupata 'bomu' yataendelea.
"Vijana ni lazima mjue kuwa wakati ukiwa masomoni unakuwa unahudumiwa kila kitu, lakini utakapokuwa umemaliza masomo utambue kuwa wazazi sasa wanakuchuulia kuwa umeshakuwa mtu mzima unayepaswa kujitegemea", alisema Jamila.
Afisa Tehama wa Makao Makuu ya CCM Levina Mkomwa akizungumza katika Kongamano la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Tawi la Chuo cha NIT, Mabibo Jijini Dar es Salaam, lililofanyika katika Chuo hicho, leo.Edgar Masatu Mjumbe na Mratibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapiduzi (UVCCM) Chuo cha NIT Mabibo Jijini Dar es Salaam akizungumza na Mratibu mwenzake wa Jumuiya hiyo kabla ya kongamano hilo kuanza.
Viongozi Meza Kuu wakibadilishana mawazo katika Kongamano hilo.
Baadhi ya Washiriki na watoa mada wakiwa kwenye Kongamano hilo.
Washiriki wakiwa kwenye Kongamano hilo
Washiriki wakiwa kwenye Kongamano hilo.
Denis Mkocha wa UVCCM NIT akizungumza kwenye Kongamano hilo.
Mhazili Msaidizi wa Chuo hicho cha NIT Jamila Mkomwa akizungumza katika Kongamano hilo.
Washiriki wakiwa kwenye Kongamano hilo.
Washiriki wakiwa kwenye Kongamano hilo.Washiriki wakiwa kwenye Kongamano hilo.Washiriki na watoa mada wakiwa kwenye Kongamano hilo.Washiriki na watoa mada wakiwa kwenye Kongamano hilo.(Picha zote na Bashir Nkoromo, CCM Blog).
No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇