Katika kura hiyo, nchi tano ikiwemo Urusi, ilipiga kura ya Hapana dhidi ya azimio hilo wakati nchi 35 hazikushiriki kura hiyo. Azimio hilo halikuwa na ulazima wa kisheria kutekelezwa, bali ni kuonyesha kutoungwa mkono kwa Urusi duniani, na halikuonekana kuwa na ushawishi wowote wa kuizuia Urusi kuendelea na vita.
Jana Jumatano, Ukraine iliwasilisha azimio jipya mbele ya kikao kingine cha dharura cha baraza kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York. Rasimu ya azimio hilo iliyoonekana na shirika la habari la AFP, linaungwa mkono na nchi 88 na awali lilikuwa limetayarishwa na Ufaransa na Mexico.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇