Mar 24, 2022

MWENYEKITI CHAMA CHA TLP AFUNGA NDOA

   Mwenyekiti wa chama cha Tanzania Labor Part (TLP), Agustino Lyatonga Mrema amesema familia ya mke wake ilimtaka alipie mahari ya Sh4.2 milioni ambapo hadi sasa ameweza kulipa  Sh1 milioni.

Mrema ambaye aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini, kuwa mbunge na kugombea urasi wa Tanzania, leo Alhamisi Machi 24, 2022 anafunga tena ndoa baada ya mke wake kufariki mwaka jana.

Mrema amesema aliwatuma wazee kwa familia ya mke wake mtarajiwa na kutakiwa kulipa kiasi hicho cha mahari.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Pages