Msimu wa Tatu wa Kampeni ya NMB MastaBata inayoendeshwa na Benki ya NMB, umezidi kushika kasi kuelekea ukingoni baada ya Alhamisi Machi 3 kufanyika kwa droo ya tisa, ambako washindi 100 walijinyakulia Sh. Milioni 10, hivyo kufanya pesa zilizopata washindi kufikia Sh. Milioni 140 kati ya Sh. Mil. 240 zinazoshindaniwa.
NMB MastaBata – Kivyako Vyako, ni kampeni inayohamasisha matumizi na manunuzi kwa njia ya kadi badala ya pesa taslimu, ambayo inaendeshwa kwa kipindi cha wiki 10, zitakazoshuhudia wateja 1,080 wakijishindia pesa taslimu Sh. Mil. 240, wakiwamo washindi 1,000 wa wiki, washindi 50 wa mwezi na 30 wa ‘Grand Finale’.
Ofisa wa Kitengo cha Kadi wa NMB, Lightness Zablon, alibainisha kuwa kampeni hiyo imekuwa na mafanikio makubwa, kwani imeongeza idadi ya miamala ya matumizi kwa njia ya kadi za MasterCard, Mastapass QR, vituo vya Mauzo (PoS) na mtandaoni.
Kampeni imeonesha mafanikio makubwa kwa kuwa imeongeza idadi ya miamala. Mwitikio wa matumizi ya kadi umekuwa mkubwa, kulingana na mahitaji ya kidijitali, ambako sasa unaweza hata kuagiza bidhaa nje ya nchini na kulipia kwa njia za kadi, badala ya pesa taslimu ambazo ni hatari kwa usalama.
Droo hiyo ilifanyika chini ya uangalizi wa Ofisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Elibariki Sengasenga, ambaye aliwahakikishia wateja wa benki hiyo kwamba kampeni hiyo inafanyika kwa kufuata vigezo, kanuni na sheria zinazotambulika na bodi yake na kuwatoa shaka wateja juu ya upatikanaji washindi.
Wakati washindi 100 wa kila wiki wakijishindia Sh. 100,000 kila mmoja, washindi 25 wa droo ya mwisho wa mwezi wa NMB MastaBasta hujishindia Sh. Milioni 1 kila mmoja, huku washindi 30 watakaopatikana kwenye ‘grande finale’ wakitarajia kujinyakulia Sh. Mil. 3, hivyo washindi 1,080 watazoa Sh. Mil. 240.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇