NAIBU Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Omari Kipanga,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi ya kukagua mradi wa ujenzi wa awamu ya pili wa Jengo la Ofisi ya Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Mtumba Jijini Dodoma leo March 2,2022 .
NAIBU Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Omari Kipanga,akizungumza mara baada ya kupokea taarifa ya mradi wa ujenzi wa awamu ya pili wa Jengo la Ofisi ya Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Mtumba Jijini Dodoma iliyosomwa na Mkadiliaji majenzi kutoka chuo cha Ardhi Bw.Saudeni Anania,wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo leo March 2,2022
NAIBU Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Omari Kipanga,akikagua mradi wa ujenzi wa awamu ya pili wa Jengo la Ofisi ya Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Mtumba Jijini Dodoma wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo leo March 2,2022
Mafundi ujenzi wa awamu ya pili wa Jengo la Ofisi ya Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Mtumba Jijini Dodoma wakiendelea na ujenzi huo.
NAIBU Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Omari Kipanga,akimsikiliza Meneja Mradi kutoka kampuni ya CRJE Bw.Li Yang wakati wa ziara ya kukagua mradi wa ujenzi wa awamu ya pili wa Jengo la Ofisi ya Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Mtumba Jijini Dodoma leo March 2,2022 .
NAIBU Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Omari Kipanga,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi ya kukagua mradi wa ujenzi wa awamu ya pili wa Jengo la Ofisi ya Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Mtumba Jijini Dodoma leo March 2,2022 .
……………………………………………………………………..
NAIBU Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Omary Kipanga amemtaka Mkandarasi anayetekeleza ujenzi wa awamu ya pili wa Jengo la Ofisi ya Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Mtumba Jijini Dodoma kampuni ya CRJE kukamilisha ujenzi huo kwa wakati.
Akizungumza Machi 2,2022 jijini Dodoma mara baada ya kukagua ujenzi wa ofisi hiyo Mtumba Naibu Waziri Kipanga amesema mradi huo unaendelea vizuri na ameridhishwa na jinsi ambavyo unatekelezwa.
Amesema wao kama Wizara watahakikisha wanausimamia mradi huo ili uweze kukamilika kwa wakati.“Nimpongeze sana Mkandarasi kwa kuweka Programu ya kazi pamoja na vitendea kazi vipo vizuri unapofanya kazi kama hii ni lazima uwe na rasilimali watu, rasilimali fedha, material,muda,menejimenti ndio maana nilihitaji kuona hivi .Tunaamini tukisimamia vizuri kazi yetu itaenda vizuri,”amesema
Amesema Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia watahakikisha wanausimamia mradi huo ili uweze kukamilika kwa wakati.
“Sisi Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia tutahakikisha tunasimamia ujenzi huu kwa kushirikiana na wenzetu wa Chuo Kikuu cha Ardhi ambao ndio washauri wa mradi ili kazi hii iweze kukamilika,”amesema.
Amesema mradi huo umeanza tangu Desemba 15 mwaka 2021 na unatarajiwa kukamilika Desemba 15 mwaka 2023 ambapo zaidi ya shilingi bilioni 15 zinatarajiwa kutumika na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameishatoa fedha hizo.
“Litakapokuwa limekamilika tunakadiria si chini ya shilingi bilioni 15 ambapo fedha hizo tayari Rais Samia Suluhu Hassan ameishazitoa kwa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia.Haya sio kwenye Wizara ya elimu tu yanajengwa katika Wizara na Taasisi zote,”amesema.
Kwa upande wake Mkadiliaji majenzi kutoka chuo cha Ardhi Bw.Saudeni Anania,amesema awamu ya pili ya ujenzi huo inajumuisha ujenzi wa jengo la ofisi lenye jumla yay a sakafu nane,sakafu ya ardhini (basement),chini (Graund Floor na za juu sita (six upper floors) ambapo sakafu ya nane ni ya kukaa mitambo ya huduma wezeshi za jengo.
Amesema pia kuna kazi za nje ambazo ni ujenzi wa maegesho ya magari,bustani pamoja na fensi ambapo amedai jengo hilo linakadiriwa kuwa na jumla ya eneo la sakafu la mita za mraba 10900.
Amesema mradi huo unaendelea vizuri ambapo utekelezaji wake umefikia asilimia 5.
“Rai yetu kwa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia kwa pamoja tunaomba juhudi zaidi katika ufuatiliaji wa malipo ya mkandarasi pindi ambapo nyaraka zinapohusu malipo zinapowafikia kutoka kwa mshauri elekezi ili kuepusha ucheleweshwaji wa mradi,”amesema.
Habari kwa hisani ya Alex Sonna-DODOMA
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇