Kitaifa maadhimisho haya yatafanyika katika Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma. Mgeni rasmi katika Matembezi ya kuhamasisha afya ya Kinywa na Meno anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa Ruvuma Brigedia.Jen Wilbert Ibuge.
kaulimbiu ni: JIVUNIE KINYWA CHAKO KWA USTAWI WA AFYA YAKO.
Mgeni rasmi katika kilele cha Maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Chama hicho Dkt. Gustav Rwekaza leo Machi 11, 2022, wakati alipokuwa akizungumza na Wanahabari (pichani hawapo) katika Ofisi ya chama hicho na pia anawakaribisha Wananchi wote wakazi wa Mkoa huo na Vijiji jirani kupata huduma bila malipo na huduma hizo ni:
Uchunguzi wa Kinywa na Meno kwenye Halmashauri (5) kati ya (8), Matibabu ya Kinywa na meno, Elimu ya afya ya Kinywa na Meno bure,
Uchunguzi na matibabu kwa Watoto wenye Mahitaji Maalum na Huduma za Kinywa na Meno kwa Mama Wajawazito na Watoto (RCH).
Pia Anawashukuru wadau kwa ushirikiano katika maandalizi ya siku hii muhimu kwa ustawi wa afya za watanzania.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇