Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe Prof. Adolf Mkenda (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe. Simai Mohamed Said ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
Pamoja na mambo mengine katika mazungumzo hayo mawaziri hao wamekubaliana kufanya kazi kwa karibu zaidi katika kupitia Sera za Elimu za Tanzania Bara na Zanzibar na mitaala ya Elimu Msingi.
Baada ya kikao hicho Mawaziri hao wamekubalina kuwa na kikao cha pamoja na wataalamu na watendaji kutoka Wizara hizo mbili kitakachofanyika Zanzibar hivi karibuni kwa ajili ya tathmini ya kazi inayoendelea ya uboreshaji Sera na Mitaala.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇