LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 23, 2022

MAANDALIZI YAPAMBA MOTO MKURABITA KURASIMISHA ARDHI KIJIJI CHA MSISI, WILAYANI BAHI+video

Meneja Urasimishaji Ardhi Vijijini kutoka Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABIT), Anthony Temu akionesha mfano wa fomu inayotakiwa wananchi kujaza majina yao, idadi ya mashamba yao, wanaopakana nao pamoja na warithi alipokuwa akitoa mafunzo ya kuwajengea uwezo wananchi wa Kijiji cha Msisi ambao ardhi yao itarasimishwa na kupatiwa hati miliki.
Temu akiendelea kutoa elimu kwa wananchi katika mkutano uliofanyika katika Kijiji cha Msisi Machi 21, 2022.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano MKURABITA, Glory Mbilimonyo akiendesha mafunzo ya kuwajengea uelewa  na uwezo wananchi wa kijiji hicho kuhusu faida za urasimishaji ardhi.
Mkuu wa Idara ya Ardhi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Wilbad Ntongani akielezea utaratibu na sheria za umiliki wa ardhi.
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Msisi, Samson Manewela akiwasihi wananchi kusikiliza kwa makini wakati wa mafunzo hayo.
Diwani wa Kata ya Msisi, Mathayo Malilo akiishukuru MKURABITA kuwapelekea mradi huo wenye manufa makubwa kwa wananchi kiuchumi.
Wananchi wakiwa makini kusikiliza wakati wa mafunzo hayo




PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA


Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Maofisa wa MKURABITA wakiendesha mafunzo hayo.....
 

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA 
MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
 0754264203

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages