WANAVIJIJI wa Jimbo la Musoma Vijijini wameendelea kutoa SHUKRANI NYINGI na za DHATI kwa SERIKALI na kwa RAIS SAMIA SULUHU HASSAN kwa kuendelea kutoa FEDHA za kuboresha MIUNDOMBINU ya BARABARA Vijijini mwao.
Zaidi ya shilingi bilioni 3.1 kutoka vyanzo mbalimbali vya fedha za serikali zilizopelekwa Musoma Vijijini zinaendelea kutumika kuboresha miundombinu ya barabara jimboni humo.
Hadi sasa FEDHA zilizowafikia kutoka Serikalini ni kama ifuatavyo:
A - Fedha za Bajeti ya Maendeleo ya Mwaka 2021/2022
Jumla Tsh MILIONI 650
B - Fedha za Jimbo
Jumla Tsh MILIONI 500
C - Fedha za Tozo
Jumla Tsh BILIONI 2
Baadhi ya barabara zinazoendelea kuboreshwa ni barabara ya kilomita 5 ya kutoka barabara kuu ya Musoma-Makojo-Busekera kwenda Kijijini Nyasaungu hadi kwenye S/M Nyasaungu
TAARIFA kutoka:
*Ofisi ya TARURA (W)
Musoma
*Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
22.2.2022
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇