LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 2, 2022

WAZIRI BITEKO AONGOZA KUTOA SOMO KWA ZIMBABWE KUHUSU MAFANIKIO YA SEKTA YA MADINI+video

Waziri wa Madini, Dotto Biteko (kushoto) akizungumza na vyombo vya habari baada ya kufanya kikao cha kubadilishana uzoefu kuhusu sekta ya madini na ujumbe wa serikali ya Zimbabwe ulioongozwa na Waziri wa Maendeleo ya Madini,Wilson Chitandoo (kulia) katika ofisi ya wizara ya madini iliyoko Mji wa Kiserikali Mtumba, Dodoma. Biteko pia ni Mwenyekiti wa nchi zinazozalisha madini aina za Almasi Afrika na Chitandoo ni Makamu mwenyekiti.
Waziri Biteko akiwa na waziri mwenzie wa Zimbabwe, Wilson Chitandoo wakati wa kikao hicho.
Ujumbe wa Zimbabwe (kulia) na ujumbe wa Tanzania ukiwa katika kikao hicho muhimu.


Waziri Biteko na Waziri wa Maendeleo ya Madini Zimbabwe, Chitandoo wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa serikali ya Zimbabwe na Tanzania. Waliokaa kulia ni Naibu Waziri wa Madini wa Tanzania, Dkt Steven Kiruswa na kushoto ni Mwanasheria Mkuu wa Zimbabwe.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt Kiruswa (kulia) na Waziri wa Madini, Dotto Biteko wakimuaga Waziri wa Maendeleo ya Madini wa Zimbabwe, Wilson Chitandoo pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Zimbabwe.


PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA


Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii video, Waziri Biteko akielezea kuhusu kikao hicho....
 

Imeandaliwa na Richard Mwaikenda 
Mhariri Blog ya Taifa ya CCM
 0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages