(1) UJENZI WA BARABARA YA LAMI
(Musoma-Makojo-Busekera)
*MRADI umechelewa sana kutekelezwa. TANROADS na WIZARA wanasahihisha mapungufu yaliyopo.
*MKANDARASI ametoa AHADI kwamba ataanza KUWEKA LAMI kipande cha KILOMITA 5 kabla ya tarehe 1.3.2022. Hatutasahau ahadi kadhaa tulizokwishapewa huko nyuma. TUFUATILIE!
(2) MAJI YA BOMBA KUTOKA ZIWA VICTORIA
(2a) MRADI WA CHITARE-MAKOJO
*Tenki la maji la ujazo wa LITA 75,000 limeishajengwa Kijijini Chitare
*Tenki la maji la ujazo wa LITA 100,000 limeishajengwa Kijijini Makojo
*MAJARIBIO yalifanyika na maji yakapatikana. Kwa bahati mbaya TRANSFOMA (100 kv) ILIUNGUA. TANESCO wanakaribia kufunga TRANSFOMA nyingine hapo.
(2c) MRADI WA SUGUTI-SARAGANA-NYAMBONO-MIKUYU
*Tenki la maji la ujazo wa LITA 200,000 limeishajengwa kwenye Kitongoji cha Nyabhelango (juu mlimani), Kijijini Nyambono.
*TRANSFOMA (200 kv) ya kusaidia kusukuma maji kutokea kwenye "booster" iliyojengwa Kijijini Chirorwe ILIUNGUA (siku moja ya ile ya Kijijini Makojo). TANESCO wanakaribia kufunga TRANSFOMA nyingine hapo kwenye "booster."
(2d) MRADI WA SUGUTI-BUGOJI-KANDEREMA-KABURABURA
*Huu ni MRADI wa FEDHA za UVIKO 19/IMF.
*Tenki la maji la ujazo wa LITA 200,000 limeanza kujengwa kwenye Kitongoji cha Nyabhelango (juu mlimani), Kijijini Nyambono.
Kwa hiyo, Kitongoji cha Nyabhelango cha Kijiji cha Nyambono kitakuwa na MATENKI 2 ya MAJI ya kusambaza kwenye VIJIJI vilivyotajwa hapo juu.
RUWASA inafanya kazi nzuri ya kusambaza maji ndani ya Jimbo letu. WANAVIJIJI wanaombwa kutoa USHIRIKIANO mzuri na mkubwa sana kwenye UTANDAZAJI wa MABOMBA ya MAJI vijijini mwao - TUNAFANIKIWA!
PICHA za hapa zinaonesha MIUNDOMBINU ya MAJI ya BOMBA ya MIRADI (2) ya kutoka Ziwa Victoria (Kijijini Suguti) kupitia Kijijini Chirorwe (Tenki lenye nyumba ndogo pembeni, kwenye "booster") hadi Mlimani Nyabhelango (kwenye Tenki lenye ujazo wa maji wa Lita 200,000). Tenki la pili la Vijiji vya Bugoji, Kanderema na Kaburabura linajengwa hapo.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇