LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 16, 2022

MWILI WA MTOTO WA MZEE MALECELA, DK. MWELE KUWASILI NCHINI KESHOKUTWA, KUAGWA DAR JUMAMOSI, DODOMA JUMATATU

Na Bashir Nkoromo, CCM Blog
Mwili wa Mtoto wa Waziri Mkuu mstaafu na Mwenyekiti Mstaafu wa Chama Cha Mapundizi (CCM) Mzee Dk. John Samuel Malecela, Dk. Mwele Ntuli Malecela aliyefariki Februari 10, 2022, mjini Geneva, Uswisi wakati akipatiwa matibabu, utarajiwa kuwasili Nchini keshokutwa, Ijumaa saa 5 asubuhi.

Taarifa iliyotolewa na familia imesema,  mwili huo utapokewa muda huo wa saa 5 asubuhi katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam na baada ya kupokewa na Ndugu, Jamaa na Marafiki utapelekwa hadi nyumbani kwa Baba wa Marehemu, Mzee Malecela eneo la Sea View ambako utalala.

Kulinagana na Taarifa hiyo, kesho yake, yaani siku ya Jumamosi asubuhi itafanyika sala fupi hapo nyumbani kwa Mzee Malecela eneo la Sea View na kisha mwili utapelekwa Kanisa la St. Albano Jijini Jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya sala itakayofanyika kuanzia saa 3 asubuhi na imekadiriwa kuwa sala hiyo kumalizika saa 5 asubuhi.

Taarifa imesema , baada ya hapo, mwili utapelekwa Ukumbi wa Karimjee kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho kwa watu wote pamoja na kutoa salam za rambirambi kutoka kwa Serikali, Mashirika na Wageni mbalimbali hadi mida ya saa 10 jioni na kisha mwili utapelekwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ajili ya kusafirishwa kwenda Dodoma.

Baada ya mwili kufikishwa Uwanja wa Ndege wa Dodoma, ambapo imekisiwa kuwa utafika saa 2 usiku, mwili utapelekwa moja kwa moja katika Hospitali ya Benjamin Mkapa ambako utahifadhiwa hadi siku ya Jumatatu, na kwamba  Jumapili waombolezaji wataendelea kupokelewa nyumbani kwa Mzee Maecela eneo la Kilimani hapo Mjini Dodoma.

"Jumatatu mwili utawasili nyumbani Kilimani Dodoma kiasi cha saa 4 asubuhi ambako itafanyika sala fupi na kisha utapelekwa Kanisa la Anglicana Dodoma kwa ajili ya sala na baadaye kupelekwa Mvumi kwa ajili ya Ibada ya maziko", imesema taarifa hiyo.

Taarifa imesema kwa watakaowiwa kutoa michango ya rambirambi kwa njia ya miamala ya simu inapokelewa kupitia namba 0717381581 Yusto Malecela na  0712 290055 Ilumbo Malecela.

                   Dk. Mwele Malecela enzi za uhai wake

Blog ya Taifa ya CCM (CCM Blog) Inaendelea pole za dhati Ndugu, Jamaa na Marafiki na wote walioguswa na Msiba huu.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages