LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 7, 2022

MAANDALIZI YA KANISA HALISI YA HIJA YA CHANZO HALISI ITAKAYOFANYIKA KIGOMA MWEZI HUU YAZIDI KUPAMBA MOTO

Na Bashir Nkoromo, Tegeta
Maandalizi ya safari ya kwenda Hija ya Chanzo Halisi cha Mungu Baba ya Kanisa Halisi la Mungu Baba, itakayofanyika mkoani Kigoma, tarehe 27 mwezi huu (26 Thebeti Majira Halisi) yamezidi kupamba moto baada Uzao (waumini) wa Kanisa hilo kuhamasika na kujitokeza kwa wingi kujiorodhesha ili kuhudhuria Hija hiyo.

Hamasa ya Uzao au waumini hao kujiorodhesha na kulipa nauli kwa ajili ya safari ya Hija hiyo, imekolezwa na Kiongozi Mkuu wa Kanisa Halisi la Mungu Baba, Baba Halisi, baada ya kufafanua kwa kina maana halisi ya Hija hiyo, katika Ibada iliyofanyika Makao Makuu ya Kanisa hilo, Tegeta Namanda Jijini Dar es Salaam, jana.

Mbali na kujiorodhesha Uzao na Makuhani kadhaa walioshiriki katika Ibada hiyo, wamejitokeza mbele ya Baba Halisi na kuwa tayari kuchangia gharama mbalimbali zitakazofanikisha Hija hiyo, ikiwemo matangazo kwenye vyombo kadhaa vya habari na kuchapisha mabango.

Kabla ya kutoa ufafanuzi kuhusu kuhusu umuhimu kila mtu kushiriki, Baba Halisi alisema Ibada kubwa ya Hija hiyo itafanyika katika Uwanja wa Lake Tanganyika Kigoma mjini kuanzia saa 8 mchana hadi saa 10 jioni, siku ya Jumapili ya tarehe hiyo ya 27, mwezi huu (26 Thebeti Majira Halisi) na itahudhuriwa hadi na watu kutoka Mataifa mbalimbali Duniani ikiwemo Marekani, Ulaya, Asia na Astralia.

"Sauti Mpya (2019) ambayo imetangaza kuwa Tanzania ni Taifa Baba ilisikika Kigoma, Tanzania; Sauti Mpya ambayo imetangaza kuwa Afrika ni Bara la Nuru ilisikika Kigoma, Tanzania; Sauti Mpya ambayo ni zaidi ya zile Sauti Saba ilisikika Kigoma,Tanzania; Sauti Mpya ambayo ni zaidi ya ishara tatu mbinguni (Ufunuo 12:1-9) ilisikika Kigoma, Tanzania na Sauti Mpya ambayo ni zaidi ya Nafsi ya Moyo (Miungu tisa mitakatifu iliyofafanuliwa ndani ya Kitabu) ilisikika pia Kigoma, Tanzania.

Sasa Kigoma, Tanzania na Afrika tujitambue kuwa tuna Sauti Mpya ambayo inabadilisha maisha mabaya kuwa mazuri, Sauti Mpya imebeba kila kitu kizuri. Hija hii ya Chanzo Halisi cha Mungu Baba  inayofanyika Kigoma, siyo maigizo wala usanii, ni halisi", alisema Baba Halisi akifafanua umuhimu wa Hija hiyo na kwa nini inabidi ifanyike Kigoma kila mwaka na kuongeza kuwa Sauti hiyo mpya sasa imepokelewa katika mabara yote kwa utukufu wa Mungu Baba.

Baba Halisi amesema kutokana na sababu hizo Watu wa Dini zote, Madhehebu yote, Makabila yote, Lugha zote, Ngazi zote, Sekta zote na Mtaifa yote wanapaswa kuhudhuria Ibada hiyo ya Hija ya Chanzo Halisi bila kukosa.

Kiongozi Mkuu wa Kanisa Halisi la Mungu Baba, Baba Halisi akionyesha mabango ambayo yatawekwa maeneo mbalimbali mkoani Kigoma, kuwandaa watu kuhudhuria Ibada kubwa ya Hija ya Chanzo Halisi itakayo fanyika mkoani humo  tarehe 27 mwezi huu (26 Thebeti Majira Halisi), Mabango hayo ameyaonyesha katika Ibada iliyofanyika leo Makao Makuu ya Kanisa hilo, Tegeta Jijini Dar es Salaam.
Baba Halisi akianza Ibada kwa Somo la 'Kujivua Moyo wa Zamani' kwa kuwaita mbele Makuhani wanaotoa huduma katika Chumba cha Fedha, ili kuweka Chanzo Halisi katika Chumba hicho.
"Sasa kwa kuwa kuanzia leo Tumejivua Moyo wa zamani, haitaitwa tena kutoa Sadaka bali Iitaitwa kutoa matunda", Akasema Baba Halisi wakati akitoa matunda yake kwenye chombo maalum, wakati wa Ibada hiyo.
Baada ya Baba Halisi kutoa madunda, ikafuatia zamu ya Makuhani na Uzao kutoa matunda. Muziki ukapigwa kusindikiza utoaji matunda👇
-----------------------------------------------------------
Kisha Baba Halisi akayabariki matunda👇
Baba Halisi akifanya shukurani ya kubariki matunda.
Makuhani wanaohudumu katika chumba cha fedha wakipokea shukrani ya kubarikiwa kutoka kwa Baba Halisi
Uzao wakipokea Baraka ya Shukurani kutoka kwa Baba Halisi. Kulia ni Mama Halisi.
Baba Halisi akimtia kichwani Maji ya Baraka (Damu Safi Nyeupe) kumbariki mmoja wa Makuhani anayehudumu katika Chumba cha Fedha, kufuatia kuvuliwa Moyo wa zamani.
Baba Halisi akimtia kichwani Maji ya Baraka (Damu Safi Nyeupe) kumbariki mmoja wa Makuhani anayehudumu katika Chumba cha Fedha, kufuatia kuvuliwa Moyo wa zamani.
Baba Halisi akimnywesha Maji ya Baraka (Damu Safi Nyeupe) kumbariki mmoja wa Makuhani anayehudumu katika Chumba cha Fedha, kufuatia kuvuliwa Moyo wa zamani.
Baba Halisi akimnywesha Maji ya Baraka (Damu Safi Nyeupe) kumbariki mmoja wa Makuhani anayehudumu katika Chumba cha Fedha, kufuatia kuvuliwa Moyo wa zamani.
Baba Halisi akimtia Maji ya Baraka (Damu Safi Nyeupe) kumbariki mtoto wa mmoja wa Makuhani anayehudumu katika Chumba cha Fedha, kufuatia kuvuliwa Moyo wa zamani.
Uzao wanaomiliki Kampuni kubwa ya PR na mmoja wa Watangazaji mahiri (kulia), wakiwa mbele kwa unyenyekevu, baada ya kuitwa na Baba Halisi ili kufuatia kuvuliwa moyo wa zamani, sasa wasiwe na woga wa kumtangaza kwenye vyombo vya habari, kama wanayofanya kwa baadhi ya wengine. Kisha Baba Halisi akiwanywesha na kuwatia kichwani Maji ya Baraka (Damu safi nyeupe) kuwabariki.👇
-------------------------------------------------------
Mama Halisi akimfurahia mtoto (kulia) wa Kuhani mmoja ambaye alikuwa akifanya 'mambo' yake wakati Ibada ikiwendelea Kanisani. Kuhani mwenye mtoto huyo alikuwa akihangaika kumtuliza kila akienda huku na huko Kanisani, lakini Baba Halisi akamwamuru amuache. "Hata akija huku ninakohubiria wewe muache tu, maana akija kwangu anajua ni mahala salama", akasema Baba Halisi.
Baadhi ya Makuhani na uzao wakiwa kwenye Ibada hiyo.
Makuhani na Uzao wakiwa kwenye Ibada hiyo.
Wasaidizi Baba na Mama Halisi wakipokea Baraka kutoka kwa Baba Halisi wakati wa somo la Kuvuliwa moyo wa zamani. Kulia ni Kaka Huduma.
Baba Halisi akimnywesha Maji ya Baraka (Damu Safi Nyeupe) Kaka Huduma Mpya.
Baba Halisi akimtia Maji ya Baraka (Damu safi Nyeupe) mmoja wa Wasaidizi hao kumpariki.  Kisha Ukafika Muda wa Baba Halisi kuhamasisha Makuhani na Uzao kuwa tayari kushiriki kwa hali na mali kufanikisha safari ya Hija ya Kigoma👇
Baba Halisi akionyesha mabango ambayo yatawekwa maeneo mbalimbali mkoani Kigoma, kuwandaa watu kuhudhuria Ibada kubwa ya Hija ya Chanzo Halisi itakayo fanyika mkoani humo  tarehe 27 mwezi huu (26 Thebeti Majira Halisi), Mabango hayo yatawekwa maeneo mbalimbali ikiwemo Ujiji, Mwanga Centre, Bigabiro, Stendi Kuu ya Mabasi Kigoma Mjini na Uwanja wa Lake Tanganyika ambako Ibada Kuu ya Hija hiyo itafanyika.
Baba Halisi akiendelea kueleza  kuhusu mabango hayo
Kisha Baba Halisi akahamasisha Makuhani wajitokeze kujitolea kuchangisha uchapaji wa mabango makubwa zaidi ya aina hiyo yatakayokuwa Kigoma.
"Haya mabango tutayachapisha makubwa kuliko haya yaliyopo hapa, sasa nataka Makutani watano waje hapa ili kila mmoja achague bango atakaloshughulikia", akasema Baba Halisi. Na Baada ya kusema hivyo makuhani zaidi ya watano wakajitokeza hara👇
👆Baada ya kujitokeza makuhani hao wakaanza kila mmoja kuchagua bango la kushughulikia, huku Baba Halisi akiwatazama wakati wakiorodheshwa na Kuhani Faida👇.
---------------------------------------------

Makuhani na Uzao ambao wamekwisha onyesha nia ya kwenda kwenye Hija hiyo lakini bado wamepungukiwa fedha ya nauli zao za treni, wakiwa mbele ya Baba Halisi baada ya kuwaita ili awafanyie Baraka wanyookewe na kukamilisha nauli hizo.
Baba Halisi akiwaombea Baraka Makuhani na uzao hao.
Baadhi ya Uzao na Makuhani wakitoa michango yao ya nauli zao za kwenda Hija hiyo.

Mama Halisi akimhudumia Maji (Damu Safi Nyeupe) Baba Halisi mwishoni mwa Ibada hiyo. Kushoto ni Kaka Halisi.

©2022 CCM Blog/Bashir Nkoromo

2 comments:

  1. Ubarikiwe mno ndugu Nkoromo kwa kumtangaza Mungu wa kweli (Chanzo Halisi).

    ReplyDelete
  2. Tunashukuru Aliyetuumba kuyajua haya .tulizoea kusikia hija Israel,Madina na Maka.leo Hija ni kigoma Tanzania.ni sisi kujitambua,kujisimamia,kujikubali.

    ReplyDelete

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages