Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka ameshiriki katika ukaguzi wa ujenzi wa Ukingo wa bahari kuzuwia eneo la bahari isingie kwenye makazi ya wananchi, ikiwa ni utekelezaji wa Ibara 192 ya ilani uchaguzi 202/2025.
Ujenzi huo umefikia asilimia 80 umegharimu jumla ya Shillingi millioni 300 ambapo hadi kukamilika T. Shs 510,286,500 zitatumika chini ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar.
Aidha Ameshiriki katika ujenzi wa Taifa Tawi la CCM Chimba na kisha kuzungumza na wanachama na wananchi katika shina no 2.
Ziara hiyo inaongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Cde Daniel Chongolo kisiwani Pemba kwa siku mbili.
#ChamaImara
#KazIndelea
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇