LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 24, 2022

PROF MUHONGO ATEMBELEA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA MUSOMA VIJIJINI


MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo akiwa na baadhi ya wanafunzi walioanza masomo ya Kidato cha Kwanza  katika Shule ya Sekondari ya Tegeruka alipotembelea  kuona wanafunzi walionza baada ya shule hiyo ambayo baadhi ya vzumba vya madarasa vimejengwa kwa fedha ya Uviko 19/IMF.


 

Profesa Muhongo akikagua moja ya vzumba vya madarasa  hayo.


Baadhi ya vyumba vya madarasa vilivyojengwashuleni hapo kwa  kwa fedha za Uviko 19




Prof Sospeter Muhongo, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini ametembelea TEGERUKA SEKONDARI akifuatilia wanafunzi waliokwisha fika shuleni hapo kuanza Masomo ya Kidato cha kwanza (2022).


Siku alipotembelea shule hiyo Januari 19, 2022 alikuta Wanafunzi 54 kati ya 184 tayari wameanza masomo ya Kidato cha Kwanza.

 Prof Muhongo amepiga PICHA na Wanafunzi hao wa Kidato cha Kwanza - baadhi ya Wazazi na Walimu.


Pia, Profesa Muhongo alikagua ujenzi wa Miundombinu kwenye Sekondari hiyo.


(i) Tegeruka Sekondari ilikuwa ya kwanza, ndani ya Jimbo hilo, kukamilisha ujenzi wa VYUMBA VIPYA 3 vya MADARASA kwa kutumia fedha za UVIKO 19/IMF zilizopatikana kwa juhudi za Mhe Rais Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. SHUKRANI NYINGI SANA kwa Mhe Rais wetu.


(ii) Sekondari haina MAABARA na MAKTABA. Mbunge wa Jimbo amekubali kutoa MICHANGO kwa kushirikiana na WANAVIJIJI wa KATA ya TEGERUKA kuanza mara moja ujenzi wa MAABARA 3 za masomo ya SAYANSI (Physics, Chemistry & Biology).


TEGERUKA SEKONDARI inahudumia VIJIJI 3, Kataryo, Mayani na Tegeruka. Ina jumla ya WANAFUNZI 509 na WALIMU 12, wakiwemo 5 wa Masomo ya Sayansi.


Ofisi ya Mbunge

Jimbo la Musoma Vijijini

www.musomavijijini.or.tz

19.1.2022

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages