LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 18, 2022

WAZIRI MKENDA: SERIKALI KUTATHMINI WAHITIMU VETA WANAOWEZA KUJIAJIRI AU KUAJIRIWA

 

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf  Mkenda akizungumza katika hafla ya kutunuku vyeti kwa Wanagenzi wahitimu wa Mpango wa Urasilimishaji Ujuzi uliopatikana nje ya Mfumo Rasmi wa Mafunzo katika Chuo cha Hoteli na Utalii VETA Njiro
Baadhi ya wahitimu wa Mpango wa Urasilimishaji Ujuzi uliopatikana nje ya Mfumo Rasmi wa Mafunzo wakipongezwa na Waziri wa Elim, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf  Mkenda baada ya kuimba shairi.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf  Mkenda na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Vijana, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu wakifurahia jambo wakati wa  Hafla ya kutunuku vyeti kwa Wanagenzi wahitimu wa Mpango wa Urasilimishaji Ujuzi uliopatikana nje ya Mfumo Rasmi wa Mafunzo katika Chuo cha Hoteli na Utalii VETA Njiro


Na Mwandishi wetu, Arusha.

SERIKALI kufanya tathimini ya wahitimu wanaomaliza katika Vyuo vya Ufundi Stadi (VETA) ili kuona namna  wanavyoweza  kujiajiri  ama kuajiriwa baada ya  kumaliza mafunzo 


Kauli hiyo imetolewa leo Januari,15  2022 jijini Arusha na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda katika hafla ya kutunuku vyeti  Wanagenzi wahitimu wa Mpango wa Urasilimishaji Ujuzi uliopatikana nje ya Mfumo Rasmi ambapo amesema mafunzo yanayotolewa ni lazima yaendane na ujuzi unaotakiwa katika soko ajira.


Prof. Mkenda amesema pamoja  na kuangalia wahitimu hao wanafanya kazi gani ama wamejiajiri wapi  pia Wizara inatarajia kuangia mtazamo wa waajiri  wa wahitumu hao na kuwataka kutoa ushauri  nini kiongezwe katika mafunzo na kipi kiwekewe mkazo ili kuwezesha VETA kutoa mafunzo yenye tija kwa vijana na Taifa.


" Tunatoa mafunzo ya VETA kwa sababu tunataka kuongeza ujuzi kwa vijana ili waweze kujiajiri na kuajirika na sio suala la idadi kwamba tunatoa vyeti kwa wahitimu wangapi au tunajenga vyuo vingapi, tunataka tuone ujuzi na taaluma wanayoipata  inatumika. Tunataka Waajiri  waanze kuulizia watu wenye vyeti vya VETA" amesisitiza Waziri huyo


Waziri huyo ameongeza kuwa hata ilani ya Chama cha Mapinduzi inataka kuongezwa kwa ajira mpya  milioni nane ifikapo 2025, hivyo vijana wanaosoma VETA wakifundishwa vizuri na kupata ujuzi stahiki wataajirika na itasaidia kuondoa mazoea ya sasa ya waajiri kutafuta wafanyajazi nje ya nchi.


Aidha  Prof. Mkenda amewataka wahitimu wa programu ya uanagenzi kutokubweteka katika hatua waliofikia ila waendelea kujisomea zaidi kwani mafunzo hayo yamewafungulia jukwaa la kupata elimu zaidi ili kuwawezesha kuendana na mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia yanayotokea Duniani


Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Vijana, Ajira, Kazi na Wenye Ulemavu Prof. Joyce Ndalichako amesema lengo kuu ya programu ya Taifa ya kukuza ujuzi ni kuwezesha nguvu kazi ya taifa  kupata ujuzi na stadi za kazi ili kumudu ushindani katika soko la ajira la ndani na nje ya nchi.


Prof. Ndalichako amesema washiriki ambao wamehitimu wamepata  mafunzo kwa kuzingatia mapungufu yaliyojitokeza wakati wanafanyiwa tathimni kutokana na ujuzi walio nao  hivyo mafunzo na vyeti walivyopota vitawawezesha kujiendeleza kielimu.


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kaspar Mmuya amesema mafunzo hayo kwa awamu tatu yameshatoa zaidi ya wahitimu elfu 20 ambao ujuzi wao umerasilimishwa na kupatiwa vyeti.

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages