Dodoma, Tanzania
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali
Mwinyi ameeleza matumaini yake kuwa, iwapo dhana ya Uchumi wa Buluu
itaeleweka vyema kutakuwa na nafasi nzuri ya kurekebisha na kuboresha
sheria na taratibu za Mahakama katika safari ya kuujenga uchumi wa
Zanzibar.
Rais
Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo Januari 23, 2022 katika Uzinduzi wa
Maadhimisho ya Wiki ya Sheria uliofanyika katika viwanja vya Nyerere
Square jijini Dodoma uliokwenda sambamba na uzinduzi wa Nembo pamoja na
Bendera ya Mahakama.
Ameeleza
kwamba kwa lugha nyingine sheria na taratibu za Mahakama zilizopo
lazima ziendane na mipango iliyopo ya Serikali yenye lengo la kuboresha
maisha ya wananchi kupitia Uchumi wa Buluu.
"Mimi
binafsi nitafurahi sana kama wanasheria kutoka pande zote mbili za
Muungano, mtakuwa na mijadala ya dhati kuhusu ni kwa kiasi gani, sheria
na taratibu za kimahakama zinavyoweza kuboresha kwa lengo la kufanikisha
dhamira ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Awamu ya Nane ya ujenzi wa
Uchumi wa Buluu,"amesema Dkt. Mwinyi.
Aidha,
Rais Dkt. Mwinyi amerejea kauli yake aliyoitoa Novemba 11,2020 katika
hotuba ya uzinduzi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar pale aliposema
kwamba Wazanzibari hawana budi kuigeuza bahari kuwa ndio shamba lao
kwani huko ndiko fursa za ajira za Zanzibar mpya zilizopo ambapo pia,
huo ndio msingi wa dhana nzima ya Uchumi wa Buluu.
Amesisitiza
kwamba Zanzibar haikujaaliwa ardhi kubwa kwani ni nchi ya visiwa ambapo
idadi ya watu wake imeongezeka mara tano katika kipindi cha miaka 56
ambapo mwaka 1964 Wazanzibari walikuwa laki 3 tu ambapo hivi sasa wapo
takribani milioni 1.6.
Katika
hotuba hiyo Rais Dkt. Mwinyi alitoa wito kwa Wanasheria na wataalamu wa
sheria, viongozi wa Mahakama na watumishi wa sekta za sheria kuielewa
na kuifanyia kazi mipango mikuu ya uchumi wa Tanzania na kuwa huru kutoa
ushauri wa kisheria Serikalini kwa lengo la kuifanikisha.
Rais
Dkt. Mwinyi amesema kuwa, Serikali zote mbili zinatambua kwamba zipo
sheria ambazo huenda zikawa ni kikwazo cha kufikia matarajio ya kiuchumi
na ustawi wa jamii ambapo sheria hizo zinahitaji kufanyiwa mabadiliko
ili zifamikishe mipango ya uchumi wa kisasa.
Hivyo,
amewahimiza wadau hao wa sheria, kutumia utaalamu wao kuzishauri
Serikali zote mbili kuchukua hatua za kurekebisha sheria ambazo zina
kasoro na kufanya hivyo kwa maslahi mapana ya Tanzania na Watanzania
wote.
Rais
Dkt. Mwinyi ameeleza kuwa kwa upande wa Zanzibar dhamira ya Serikali ya
kujenga uchumi wa kisasa unaozingatia matumizi sahihi ya rasilimali za
bahari au kama unavyofahamika Uchumi wa Buluu, ambazo ni jitihada za
dhati kabisa za kujenga uchumi utakaowasaidia wananchi wa Zanzibar.
Alieleza
kwa upande wa pili ambako kuna dhamira ya Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ya kupunguza umaskini na kuwa na uchumi unaolingana
na ushindani wa Karne ya 21.
Kutokana
na juhudi hizo, Rais Dkt. Mwinyi alieleza kwamba ni dhahiri kuwa
kufanikiwa kwa dhamira na jitihada hizo za Serikali zote mbili
kutategemea uwezeshaji na mchango mkubwa wa sekta ya sheria na hasa
kupata ushauri wa kutoka kwa wanasheria wa hapa nchini.
Alieleza
kwamba amekuwa akisisitiza umuhimu wa kuheshimu sheria kwa vile
anatambua kuwa miongoni mwa mambo yanayodhoofisha misingi ya utawala
bora ni kuwepo wka vitendo vya rushwa, ubadhirifu,uzembe,kukosa
uwajibikaji na kutofuata sheria na kukiuka kwa maadili.
"Nafahamu
kwamba sheria ina umuhimu mkubwa katika kujenga umoja wetu,amani yetu,
udugu wetu, na pia mshikamano wetu, mafanikio ya kiuchumi, kibiashara na
kiuwekezaji hutegemea kuwepo kwa misingi ya utawala wa sheria na uhuru
wa Mahakama,"amesema Dkt.Mwinyi.
Aidha,
Rais Dkt. Mwinyi alieleza kuridhishwa na hatua ya ushirikiano iliyopo
baina ya Mahakama ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mahakama ya
Zanzibar ambapo uhusiano huo ni wa muda mrefu tokea mwaka 1965.
"Nafurahi
kuona kuwa ushirikiano huo unaendelezwa kwa kupeana uzoefu na utaalamu
utakaoongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yetu hivyo natoa
wito kuendeleza kwa lengo la kuwa chachu ya kuleta mabadiliko ya
utendaji na kuongeza kasi ya ufanisi katika mahakama zetu," amesisitiza
Dkt. Mwinyi.
Naye
Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Profesa Ibrahim Hamis
Juma alieleza kwamba Wiki ya Sheria itakuwa na mambo mbalimbali ya
kisheria hadi tarehe 29 na siku ya Sheria itakuwa Februari 1,2022 ambapo
mgeni rasmi atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia
Suluhu Hassan.
Amewakaribisha
wananchi kwenda katika maonyesho hayo yaliyozinduliwa na Rais
Dkt.Mwinyi ili waweze kupata mahitaji yao mbali mbali ya kisheria.
Jaji
Mkuu huyo ametumia fursa hiyo kumpongeza Rais Dkt.Mwinyi kwa kuimarisha
sheria ikiwa ni pamoja na kuimarisha Uchumi wa Buluu ambao utahitaji
mabadiliko ya sheria huku akiahidi ushirikiano mkubwa katika kuhalikisha
dhana hiyo inafikia malengo yaliyokusudiwa sanjari na kuimarisha
mashirikiano ya Kimahakama kati ya pande mbili hizo.
Pia,
aliwasisitiza wananchi kuwa na utamaduni wa kujisomea hasa katika
sheria huku wakiwataka wajitayarishe kwa kutumia mfumo wa akili bandia”
katika kutoa ushauri wa kisheria jambo ambalo linakwenda na wakati
uliopo hivi sasa pamoja na kupunguza kharama za kuendeshea kesi.
Mapema
asubuhi, Rais Dkt. Mwinyi aliongoza matembezi ya kilomita saba
yaliyoanzia katika viwanja vya Kituo Jumuishi cha Haki, Jijini Dodoma na
kupita katika maeneo mbali mbali na hatimae kuishia katika viwanja vya
Nyerere Square ambapo Mama Maria Mwinyi nae alishiriki kikamilifu.
Baada
ya kufika katika eneo hilo la uzinduzi huo, Rais Dkt. Mwinyi
alitembelea mabanda ya maonyesho pamoja na kuzindua rasmi bendera na
Nembo ya Mahakama.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali
Mwinyi akiondoa kipazia kuashiria kuizindua Nembo ya Mahakama Kuu
Tanzania wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Wiki ya Sheria Tanzania
iliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma huku akiwa
na Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Hamis Juma.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi akihutubia na kufungua Wiki ya Sheria Tanzania
iliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.Baadhi
ya Majaji wa Mahkama Kuu Tanzania wakifuatilia
hotuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk.
Hussein Ali Mwinyi akihutubia na kufungua Wiki ya Sheria Tanzania
iliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Wageni waalikwa wakifuatilia hituba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani)
akihutubia na kufungua Wiki ya Sheria Tanzania iliyofanyika katika
viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein
Ali Mwinyi akifanya mazoezi ya viungo katika viwanja vya Kituo Jumuishi
cha Utoaji Haki Dodoma, kabla ya kuaza kwa Matembezi ya Ufunguzi wa Wiki
ya Sheria na (Kushoto kwa Rais) Jaji Mkuu wa Tanzania Prof Ibrahim
Hamis Juma na (kulia kwa Rais) Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Mhe Dkt.
Tulia Ackson , Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi, wakiwa na
Viongozi wengine wa Serikali na Mahakama.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein
Ali Mwinyi akiwa katika matembezi ya Ufunguzi wa Wiki ya Sheria Tanzania
inayofanyika Jijini Dodoma katika viwanja vya Nyerere Square Jijini
Dodoma na (kushoto kwa Rais) Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe.Prof Ibrahim
Hamis Juma na Kaimu Jaji Mkuu wa Zanzibar Khamis Ramadhan Abdalla na
(kulia kwa Rais) Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Mhe Dkt. Tulia Ackson,
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma
Mhe.Anthony Mtaka, wakishiriki katika matembezi hayo yalioazia Kituo
Jumuishi cha Utoaji Haki Dodoma na kumalizika katika viwanja vya Nyerere
Square Dodoma
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein
Ali Mwinyi akifanya mazoezi baada ya kumaliza matembezi ya Ufunguzi wa
Wiki ya Sheria Tanzania yalioazia katika Kituo Jumuisho cha Utoaji Haki
na kumalizia katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma na (kushoto
kwa Rais) Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma na Kaimu Jaji
Mkuu wa Zanzibar Mhe.Khamis Ramadhan Abdalla na (kulia kwa Rais) Naibu
Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Mke wa Rais wa
Zanzibar Mama Mariam Mwinyi, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka
na Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe.George Boniface Simbachawene.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein
Ali Mwinyi akitembelea maonesho ya Ufunguzi wa Wiki ya Sheria Tanzania,
katika banda la Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA)
akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mradi Bi. Asha Hassan Komba na (kulia
kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na Jaji Mkuu wa
Tanzania Mhe.Prof Ibrahim Hamis Juma, maonesho hayo yanafanyika katika
viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein
Ali Mwinyi akitembelea banda la maonesho la Mamlaka ya Usimamizi wa
Bandari Tanzania (TPA) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Huduma
za Sheria,Bw.Stanislavs Kagisa na (kulia kwa Rais) Mke wa Rais Zanzibar
Mama Mariam Mwinyi, Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Hamis Juma
na Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe.George Boniface Simbachawene.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali
Mwinyi akitembelea banda la maonesho la Wizara ya Katiba na Sheria
akipata maelezo kutoka kwa Dk. Anne Malipula na (kulia kwa Rais) Mke wa
Rais Zanzibar Mama Mariam Mwinyi, Jaji Mkuu wa Tanzania Prof.
Ibrahim Hamis Juma, wakati wa ufunguzi wa Wiki ya Sheria Tanzania
yanayofanyika katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇