Jan 12, 2022

RAIS DK. MWINYI AONGOZA SHERERE ZA KILELE CHA MAADHIMISHO YA MIAKA 58 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR, LEO

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi aisalimia Wananchi alipoingia katika Uwanja wa Amaan jijini Zanzibar kuongoza Sherehe za kilele cha Maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi akipokea salamu ya Heshima ya Gwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama katika Uwanja wa Amaan jijini Zanzibar  wakati wa Sherehe za kilele cha Maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, leo.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Marium Mwinyi (katikati) Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar  Mhe.Othman Masoud Othman (kulia) Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Tulia Akson wakisimama wakati wa kupokea Salamu ya Heshma ya Gwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama katika kilele cha Maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar hafla iliyofanyika leo katika Uwanja wa Amaan Studium  jijini Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi akikagua Gwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama katika Uwanja wa Amaan jijini Zanzibar  wakati wa Sherehe za kilele cha Maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, leo. (Picha na Ikulu, Zanzibar)

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Pages