LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 24, 2022

MWILI WA MZEE JOHN NCHIMBI WAWASILI NYUMBANI, LEO, WAOMBOLEZAJI WAUPOKEA KWA VILIO

Gari lenye mwili wa Baba wa Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, Marehem Mzee John Nchimbi likiwasili nyumbani kwa marehemu, Tabata jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika kesho katika Makaburi ya Kinondoni pia jijini Dar es Salaam. Mzee John Nchini alifariki Dunia usiku wa kuamkia jana, katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) wakati akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa moyo uliokuwa ukimsumbua kwa muda mrefu.
Waombolezaji wakiwa tayari kulishusha jeneza.
Waombolezaji wakishusha jeneza lenye mwili wa Mzee John Nchimbi.
Waombolezaji wakibeba jeneza kuliingiza ndani
Waombolezaji wakiwa wamelibeba jeneza lenye mwili wa Mzee John Nchimbi kwa ajili ya kulipekea katika chumba maalum ambamo litalala kabla ya mazishi kesho.
Padri James Ngonyani wa Kanisa Katoliki akiongoza sala fupi baada ya mwili kuingizwa kwenye chumba maalum
 
Nyumbani kwa Mzee John Nchimbi

Waobolezaji wakiwa msibani
Bakari Machumu wa Mwananchi Communication akisaini kitabu cha maombolezo
Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na Padri James Ngonyani (aliyemshika begani) na Katekista Lyimo, waliofika kwa ajili ya kupokea na kuombea mwili wa marehemu Mzee John Nchimbi.
Baadhi ya waombolezaji wakiwa kwenye msibani
Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na waombolezaji kutoka Mwananchi Communication ambao Ofisi yao ipo jirani na nyumbani kwa marehemu Mzee John Nchimbi.
Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na Kada wa CCM Asaa Simba aliyefika kumpa pole.
Kada wa CCM Asaa Simba akisaini kitabu cha maombolezo
Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na baadhi ya waombolezaji waliofika kumpa pole kwa kufiwa na Baba yake.
Kijana wa UVCCM akigawa sare maalum zitakazovaliwa na waombolezaji wakati wa Ibada ya mazishi kesho
Baadhi ya waombolezaji wakitazama sare baada ya kugawiwa
Baadhi ya waombolezaji wakiwa msibani
Balozi Dk. Nchimbi akimsindikiza mmoja wa waombolezaji aliyefika kumpa pole.

Mmoja wa Watoto wa Marehemu Mzee John Nchimbi (Wanne kushoto) akiwa na baadhi ya waombolezaji waliofika kuifariji familia ya marehemu.
Baadhi ya waombolezaji
Waombolezaji wakiwa msibani.
Katibu Mkuu wa UWT Phills Nyimbi (kushoto) akiwa na viongozi wengine wa Jumuiya hiyo, kwenye msiba huo. Kulia nu Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Angel Akilimali na Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kinondoni Anna Hangaya au Mama Makete.

Katibu Mkuu wa UWT Phills Nyimbi akiteta jambo na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Angel Akilimali (kulia) wakati wakiwa kwenye msiba huo. Kushoto ni Katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam. 

Ratiba ya mazishi kesho hii hapa👇

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages