LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 8, 2022

MBUNGE MAHAWANGA 'APIGA MWINGI', AKAMILISHA USAJILI WA VIKUNDI VYA WANAWAKE WAGONGA KOKOTO, KUNDUCHI, AMPONGEZA RAIS SAMIA KWA KUSIMAMIA VEMA UCHUMI

Kunduchi, Dar es Salaam
Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Dar es Salaam kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Janeth Mahawanga amezidi kuonyesha dhamira yake ya kumkomboa Mwanamke wa mkoani Dar es Salaam kiuchumi,kufuatia kukabidhi vyeti vya usajili na uandikishwaji wa vikundi sita vya Wanawake na Vijana wenye ulemavu wanaojishughulisha na ujasiriamali wa kugonga kokoto katika Kata ya Kunduchi.

Pamoja na kuwakabidhi vyeti vya Usajili na kuandikishwa katika hafla hiyo iliyofanyika Jumanne wiki hii, Mbunge Janeth amewafungulia Akaunti za Benki kwa ajili ya kukamilisha mchakato wa kupata mkopo Wanawake hao.


Vikundi hivyo ambavyo Mbunge Mahawanga amevisaidia kupata usajili na kufungua Akaunti ni Meko Women Group, Waku Women Group, Hakuna Matata Women Group, Jasiri Women Group na cha Vijana wenye ulemavu cha Tunaweza Disability Group.

 
Hatua hiyo imekuja kufuatia ziara aliyoifanya Mbunge huyo Oktoba 8, 2021 kwenye mitaa mbalimbali iliyopo Kata hiyo ya Kunduchi ambapo aliguswa sana na wanawake ambao wanaponda kokoto kwa kutumia vifaa duni na hivyo kujipatia fedha kidogo ambazo hazitoshelezi kwa matumizi binafsi hivyo akaona ni vyema kuwapa elimu ya Vikundi, usajili na fursa ya mikopo.

Mbunge Janeth alihakikisha elimu hiyo inaeleweka kisha akaungana nao kutengeneza Vikundi, kuvisajili na kuungana na Benki ya CRDB kuhakikisha amevifungulia akaunti kupitia Benki hiyo vikundi vyote sita kimoja kikiwa nicha Vijana wenye Ulemavu ambao nao wanafanya shughuli za kugonga kokoto.

Akizunguma katika hafla hiyo Mbunge Janeth amewaahidi kuwa hatua ya mwisho ameishaitekeleza ambayo ni kuandaa maandiko ya miradi kwa ajili ya Vikundi hivyo ili kupata  mikopo ya asilimia 10% inayotolewa kwenye kila Halmashauri na kwamba atahakikisha wanapata mikopo hiyo ili waweze kujikwamua kiuchumi kama jinsi ilivyo dhamira yake ya kumkomboa Mwanamke wa mkoani Dar es Salaam kiuchumi.

Amewashukuru Benki ya CRDB kwa kukubali kujumuika nao kutoka Ofisini na kuwafuata kinamama hao ili kuwafungulia akaunti lakini pia amewapongeza wanawake wote waliojitokeza  kwa namna ambavyo wameendelea kushirikiana naye na kusisitiza ataendelea kuwa pamoja nao mpaka kuhakikisha lengo kuu la kumkwamua mwanamke kiuchumi linafanikiwa.

Mbunge Janeth amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo anaendelea kufanya kazi kuhakikisha Tanzania inapata maendeleo na amesisitiza kuendelea kumuunga mkono kwa kuhakikisha anatekeleza vyema Ilani ya CCM 2020/25 hasa kwenye suala la kuwainua wanawake kiuchumi kupitia mikopo ya Halmashauri na wadau mbalimbali wa maendeleo.
  

#TishaMama
#ItazameDarKiutofauti
#Kaziiendelee

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Dar es Salaam kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Janeth Mahawanga akikabidhi cheti cha Usajili kwa Kikundi cha Nguzo Imara Women Group ambao ni miongoni vya Vikundi 6 vya Kinamama ambao ni wajasiriamali wa kugonga kokoto katika Machimbo ya Meko, Kunduchi.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Dar es Salaam kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Janeth Mahawanga (katikati)akiwa na Maofisa wa Benki ya CRDB Tawi la Holland House, wakati akivingiulia Akaunti Vikundi vya Wajasiriamali Kinamama wagonga Kokoto.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Dar es Salaam kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Janeth Mahawanga akizungumza na Viongozi wa Vikundi 6 vya Kinamama wagonga Kokoto ambavyo vimekamilisha usajili na kufungua Akaunti akiwaeleza kuwa hatua inayofuata ni kuandaa maandiko ya miradi ambayo ameshaikamilisha hivyo kilichobaki ni kuwasilisha maandiko hayo Halmashauri kwa kuwa ilikuwa inasubiriwa kufungua Akaunti Benki. 

Mbunge huyo aliwataka kutokata tamaa akiwaasa kuwa mafanikio hayataki uvivu wala lele mama na kwamba ni Wajibu wao kuonyesha ushirikiano kama walivyomuonyesha mwanzo tangu hatua ya kuwapa elimu ya Vikundi, Fursa na Mikopo hivyo waendelee na moyo huo, yeye yupo nao kuhakikisha azma yake ya kuwakomboa Kiuchumi Wanawake wa Dar es Salaam inafanikiwa.

Mwenyekiti wa Kikundi cha Jasiri Women Gruop akiweka alama ya dole gumba kwenye fomu ya kufungulia Akaunti
Kinamama wa vikundi 6 wakitoa neno la shukrani kwa Mbunge Janeth Mahawanga kwa kutimiza ahadi yake ya kutoa elimu ya Vikundi, Fursa, mitaji na urejeshaji mikopo kuwasimamia hadi kufikia hatua waliyofikia
Viongozi wa Vikundi vya wenye ulemavu cha Tunawea Disability Gruop wakiwa katika dawati la kufungua Akaunti mbele ya Maofisa wa Benki ya CRDB na Mbunge Janeth Mahawanga. Maofisa hao wa CRDB ni Diana Jekela, Joseph Joseph na Harron Dava.
Mbunge Janeth Mahawanga akiwa katika Picha ya kumbukumbu na viongozi wa Vikundi 6 vya Kinamama waponda Kokoto baada ya usajili wa vikundi hivyo na kufungua Akaunti Kivundi hivyo ni Meko Women Group, Waku Women Group, Hakuna Matata Women Group, Jasiri Women Group na Tunaweza Disability Group. Picha kwa Hisani ya Mbunge Janeth Mahawanga

©2022 CCM Blog/Bashir Nkoromo

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages