LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 23, 2022

MAVUNDE AWATAKA BODI YA SUKARI KUTEKELEZA MIKAKATI YA KUONGEZA TIJA KWA WAKULIMA WADOGO

Na Mwandishi Maalum, Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Kilimo, Anthony Mavunde ameitaka Bodi ya Sukari kuhakikisha inasimamia kwa weledi mpango mkakati wa kuwawezesha wakulima wadogo kuzalisha miwa kwa tija. 


Mavunde ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam, jana, Januari 22, 2022,  wakati akizungumza na Wafanyakazi wa Bodi ya Sukari, alipofanya ziara ya kutembelea Bodi hiyo.

 

"Bado tunayo fursa kubwa ya kuwatumia wakulima wadogo katika kuongeza uzalishaji wa miwa nchini kwa kuwaunganisha na Taasisi za fedha, kuendeleza miundombinu ya umwagiliaji na kuwa kusanya katika vikundi na kuwahamasisha kuanzisha viwanda vidogo vya kuzalisha sukari.


Kwa sasa tija ya uzalishaji wa miwa kwa wakulima wadogo ni wastani wa tani 47 kwa hekta, wakati wakulima wakubwa ni wastani wa tani 87 kwa hekta. Hivyo, tunalo jukumu la kuhakikisha tunawasimamia wakulima wadogo wa miwa kuongeza tija ili waweze kupata kipato zaidi", Alisema Mavunde. 


Mavunde aliwataka watumishi wa Bodi ya Sukari kuwa wabunifu katika utendaji kazi wa majukumu yao na kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kutumia ujuzi na maarifa yao kuishi maono ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kukuza sekta ya sukari nchini.


Akitoa maelezo ya awali Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Prof. Kenneth Bengesi amemueleza Naibu Waziri Mavunde kwamba Bodi imejipanga kuhakikisha kwamba inawasimamia wakulima wa miwa  nchini kuongeza tija katika kilimo kwa kusimamia upatikanaji wa mbegu safi,kuboresha miundombinu ya umwagiliaji na kuwaunganisha na Taasisi za Fedha nchini.

Naibu Waziri wa Kilimo, Anthony Mavunde (Kulia), akizungumza na Watumishi wa Bodi ya Sukari, Jijini Dar es Salaam, jana.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages