Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo (Wa sita kushoto), akiwa na viongozi mbalimbali wa CCM na Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakati wakiuaga mwili wa Marehemu Madgalena Shigela, mke wa Mkuu Wa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Komredi Martine Shigela nyumbani kwa Mkuu wa mkoa huyo, Salasala Jijini Dar es Salam, jana, kabla ya mwili kusafirishwa kwenda Kishapu, Shinyanga kwa ajili ya maziko. Mbele ya Jeneza ni Komred Shigela na Wanafamilia yake.
Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo alipokuwa akiwasili msibani, nyumbani kwa Mkuu wa mkoa wa Morogoro Comredi Martine Shigela, Tegeta Salasala jijini Dar es Salaam. Wapili Kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka na kulia ni Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Mstaafu Erasto Sima na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete ambao walimpokea Chongolo.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka alipokuwa akisalimiana na Naibu Waziri Ridhiwani Kikwete baada ya kuwasili msibani.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka akikaribishwa na Katibu Mkuu Mstaafu wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Erasto Sima. Kushoto ni Naibu Waziri Ridhiwani Kikwete.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo akisaini Kitabu cha maombolezo baada ya kuwasili msibani
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka, akisaini Kitabu cha maombolezo baada ya kuwasili msibani.Waziri wa Madini Dotto Biteko akisaini Kitabu cha maombolezo baada ya kuwasili msibani.Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwan Kikwete akisaini Kitabu cha maombolezo baada ya kuwasili msibani.Mwandishi/Mpigapicha wa Michuzi Blog Ndugu Imma akisaini Kitabu cha maombolezo baada ya kuwasili msibaniKatibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo akimpa pole Comredi Shigela.Mzee Steven Wasira akimpa pole Komredi Shigela
Naibu Waziri Ridhiwan Kikwete akimpa pole Komredi Shigela.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tanga Henry Shekifu akimpa pole Komredi Shigela.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniele Chongolo akizungumza maneno ya faraja na Komredi Shigela.
Mkuu wa mkoa mstaafu Said Meck Sadick akizungumza maneno ya faraja na Komredi Shigela
Naibu Waziri Ridhiwan Kikwete akimfariji Komredi Shigela.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvivi Abdallah Ulega akizungumza maneno ya faraja na Komredi Shigela.
DC Zainab Kawawa akimfariji Komredi Shigela.
Komredi Shigela akiwa na watoto wake huku akionekana kujawa na huzuni kuu. Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo na Kulia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Godwin Gondwe (kulia) akishauriana jambo na Mkuu wa mkoa wa Pwani Aboubakar Kunenge msibani hapo.
Viogozi na waombolezaji mbalimbali wakiwa nyuma ya Komredi Shigela katika msiba huo.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Christina Mndeme akizungumza kwa niaba ya CCM katika Msiba huo.
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akizungumza kwenye msiba huo.
Komredi Martine Shigela akizungumza maneno ya shukurani kwa kufarijiwa na Viongozi wa Chama na Serikali na wananchi mbalimbali katika msiba huo.
Komredi Martine Shigela akiwa na familia yake wakati akijiandaa kwenda kutoa heshima za mwisho kwenye mwili wa marehemu mkewe.
Komredi Martine Shigela akienda na familia yake kutoa heshima za mwisho kwenye mwili wa marehemu mkewe. Kushoto ni Msanii Steve Nyerere akimuongoza.
Komredi Shigela akiwa na familia yake mbele ya Jeneza lenye mwili wa marehemu kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo akiwa na viongozi mbalimbali wa CCM na Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakati wakiuaga mwili wa Marehemu Madgalena Shigela mke wa Mkuu Wa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Komredi Martine Shigela nyumbani kwa Mkuu huyo wa mkoa, Salasala Jijini Dar es Salam, kabla ya mwili kusafirishwa kwenda Shinyanga kwa ajili ya maziko Wilayani Kishapu.
Msimamizi Mkuu wa Blog ya Taifa ya CCM Bashir Nkoromo, kwa niaba ya timu nzima anatoa pole za dhati kwa Comredi Martini Shigela, Wanafamilia na wote walioguswa kwa namna yoyote na Msima huu.
©2022 CCM Blog/Bashir Nkoromo
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇