LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 21, 2022

MAKAMU WA RAIS DK. MPANGO AONGOZA KUAGWA MWILI WA KAKA YAKE ASKOFU MSTAAFU GERALD MPANGO LEO JIJINI DAR ES SALAAM

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Philip Mpango akitoa heshima za mwisho kwa mwiliwa Kaka yake, Askofu mstaafu wa Kanisa la Anglikana Askofu Gerald Mpango wakati wa ibada ya kuaga mwili huo iliyofanyika katika Kanisa la Anglikana la  Mtakatifu Albano lililopo Posta jijini Dar es Salaam, leo Januari 21, 2022. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

 

Dar es Salaam, leo

Mwili wa Askofu Mstaafu wa Kanisa la Anglikana Gerald Mpango ambaye ni Kaka wa Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango umeagwa leo Januari 21, 2022, katika Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano  Posta Jijini Dar es Salaam.

Ibada ya kuaga mwili huo imeongozwa na Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam Jackson Sosthenes.

Akimzungumzia Askofu Gerald Mpango enziza uhai wake, skofu wa Dayosisi ya Ziwa Rukwa Mathayo Kasagala amesema daiama kanisa litakumbuka mchango wa Askofu Mpango katika kuliendeleza Kanisa ikiwemo kuanzishwa kwa Dayosisi ya Ziwa Rukwa.

Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya familia Makamu wa Rais Dkt. Philip pango ametoa shukrani zake kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa msaada pamoja na neno la faraja katika kipindi cha msiba huu.

Mwili wa Askofu Mstaafu Gerald Mpango umesafirishwa kuelekea mkoani Kigoma ambapo mazishi yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi tarehe 22 Januari 2022 wilayani Kasulu.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages