Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi zawadi ya Sh. 500,000, mwanariadha wa zamani Gidamis Shahanga ikiwa ni ishara ya kutambua heshima kubwa aliyolipatia taifa letu kwa kuwa mshindi pekee wa medali mbili za dhahabu katika mashindano ya Jumuiya ya Madola (Commonwealth Games), mwaka 1978 na 1982 mita 10,000. Mheshimiwa Majaliwa alitoa zawadi hiyo baada ya kuweka jiwe la msingi la Mradi wa Maji wa Mogitu – Katesh wilayani Hanang na kuwasalimia wananchi katika viwanja vya Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Katesh, Januari 23, 2022. Kushoto ni Naibu Waziri wa Michezo na Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pauline Gekul.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkpatia ufunguo wa pikipiki ya miguu mitatu (guta), Emmanuel John alipokabidhi pikipiki na guta kwa kikundi cha vijana kilichonufaika na mkopo wa asilimia 10 kutoka Halmashauri ya wilaya ya Hanang' akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua shughuli za maendeleo mkoani Manyara. Tukio hilo lilifanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Katesh wilayani humo, Janauri 23, 2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇