KISIWA cha Rukuba kilichopo Jimbo la Musoma Vijijini kinazidi kung'ara kimaendeleo ambapo ndani ya miaka 6 kimekamilisha yafuatayo:
(1) SHULE YA MSINGI:
*Vyumba vya Madarasa vipo vya kutosha na ziada ya chumba kimoja
(2) MAKTABA YA SHULE YA MSINGI:
*Wakazi wa Kisiwani humo walishirikiana na Mbunge wao Prof Sospeter Muhongo kujenga MAKTABA na kuweka VITABU vya kutosha.
(3) NYUMBA ZA WALIMU:
*Mdau wa Maendeleo Kisiwani humo alishirikiana na Wakazi wa Kisiwa hicho kujenga nyumba za Walimu. Kila Mwalimu amepewa nyumba ya shule, na ipo moja ya ziada.
(4) UMEMEJUA (solar):
*Mradi umeanza kutekelezwa wa utumiaji wa "solar". Zahanati inatumia "solar"
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇