Seka Sekondari ilifunguliwa mwaka jana (Julai 2021) na sasa ina WANAFUNZI wa Kidato cha Kwanza na Pili.
Sekondari hii ni ya PILI ya Kata ya NYAMRANDIRIRA ambayo ujenzi wake ulianza kwa MICHANGO kutoka kwa:
(i) Wanavijiji: fedha taslimu na nguvukazi
(ii) Mbunge wa Jimbo: fedha zake binafsi
(iii) Mfuko wa Jimbo: fedha za Serikali
(iv) Baadhi ya Wazaliwa wa Kata ya Nyamrandirira
*DAFTARI lenye orodha ya MICHANGO limetunzwa na Serikali ya Kijiji cha Seka.
KATA hii ya Nyamrandirira yenye VIJIJI 5 (Chumwi, Kaboni, Kasoma Mikuyu na Seka) kwa sasa inazo SEKONDARI MBILI (2) ambazo ni:
*Seka Sekondari
*Kasoma Sekondari yenye "HIGH SCHOOL" ya Serikali.
Tafadhali wasikilize, WANAVIJIJI na VIONGOZI wao wakimshukuru Rais wetu, Mhe Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia FEDHA za kujenga vyumba vipya 4 vya Madarasa kwenye Sekondari yao mpya.
"CLIP" imeambatanishwa hapa - tafadhali isikilize.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇