Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameimwagia sifa kampuni ya kizalendo ya ujenzi ya Mohammed Builders kwa kujenga kwa ustadi mkubwa kitega uchumi cha Jiji la Dodoma eneo la Mji wa Kiserikali, Mtumba. Majaliwa ametoa sifa hizo alipokagua mradi na kuweka jiwe la msingi katika kitega uchumi hicho ambacho kina ukumbi mkubwa wa kisasa wa mikutano na hoteli yenye hadhi.
Pichani, Waziri Mkuu Majaliwa akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mohammed Builders, Taher Jafferji ndani ya ukumbi wa kisasa wa mikutano wa kitega uchumi hicho.
Sehemu ya kuingilia kwenye ukumbi wa mikutano.
Mkandarasi Mshauri wa Ujenzi wa kitega uchumi hicho, Rose Nestory wa Kampuni ya Arges Africa Ltd, akielezea mbele ya Waziri Mkuu Majaliwa kuhusu hatua ambayo ujenzi wa kitega uchumi ulipofikia.
Waziri Mkuu, Majaliwa akikagua ukumbi wa kisasa wa mikutano.
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza/kuona kupitia clip hii ya video,Waziri Mkuu akikagua ujenzi na kuelezea jinsi alivyo furahishwa na ujenzi wa kitegauc humi hicho pamoja na kuimwagia sifa kampuni ya Mohammed Builders inayojenga...
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDAMHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇