Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisogeza kitambaa kuashiria uwekaji wa jiwe la Msingi Ujenzi wa Miundombinu ya Mabasi yaendayo Haraka Awamu ya pili (BRT II) katika Barabara ya Kilwa-Chang’ombe-Sokoine na Kawawa katika sherehe zilizofanyika Mbagala Mkoani Dar es Salaam leo tarehe 04 Desemba, 2021. Wa kwanza kulia ni Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa, Wengine katika picha ni Waziri wa TAMISEMI Ummy Mwalimu, Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akizungumza na Wananchi wa Mbagala hawaonekani pichani mara baada
ya kuweka jiwe la msingi mradi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Mabasi
yaendayo Haraka Awamu ya pili (BRT II) katika Barabara ya
Kilwa-Chang’ombe-Sokoine na Kawawa zilizofanyika Mbagala mkoani Dar es
Salaam. PICHA NA IKULU
Moja ya Kituo Kikubwa cha Mabasi yaendayo Haraka Awamu ya pili (BRT II) kilichopo Mbagala mkoani Dar es Salaam.
Sehemu ya Wananchi waliohudhuria sherehe za uwekaji wa jiwe
la msingi mradi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Mabasi yaendayo Haraka
Awamu ya pili (BRT II) katika Barabara ya Kilwa-Chang’ombe-Sokoine na
Kawawa zilizofanyika Mbagala mkoani Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Rogatus Mativila wakati
akitoa maelezo ya Ujenzi wa Miundombinu ya Mabasi yaendayo Haraka Awamu
ya pili (BRT II) katika Barabara ya Kilwa-Chang’ombe-Sokoine na Kawawa
kabla ya kuweka jiwe la msingi Ujenzi wa Mradi huo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipiga makofi pamoja na viongozi
Wengine mara baada ya kuweka jiwe la msingi Ujenzi wa Miundombinu ya
Mabasi yaendayo Haraka Awamu ya pili (BRT II) katika Barabara ya
Kilwa-Chang’ombe-Sokoine na Kawawa katika sherehe zilizofanyika Mbagala
Mkoani Dar es Salaam leo tarehe 04 Desemba, 2021.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇