LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 28, 2021

RAIS SAMIA: WALIODHANI MIRADI ITASIMAMISHWA ILI WAPATE LAKUSEMA HALIPO

CCM Blog, Ikulu

Rais Samia Suluhu Hassan amefunguka na kusema kama baadhi ya watu walidhani miradi itasimamishwa ili wapate la kusema hilo halipo.


Rais Samia, amesema hayo leo, Ikulu Jijini Dar es Salaam, wakati utiaji Saini Mkataba wa Mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha Makutupora (Singida) hadi Tabora chenye urefu wa Kilometa 368 katika kipande cha tatu cha mradi huo (Lot III).


Utiaji wa Mkataba huo umefanywa na Mkurugenzi Mkuu Shirika la Reli nchini (TRC) Masanja Kadogosa akiweka saini na Makamu Mwenyekiti wa Kampuni ya Yapi Merkez ya Uturuki Erdem Arioglu na yeye Rais Samia kushuhudia.


"Tutaendelea na ujenzi wa miradi, kuna jitihada za kutuvunja moyo kwenye mikopo, hakuna nchi isiyokopa hata hizo zilizoendelea wana mikopo mikubwa kuliko ya kwetu, tutakopa ili tumalize miradi ya maendeleo. 


Ukikopa unajenga kwa haraka, ukisubiri ukusanye za kwako utamaliza lini kujenga, na wakopwaji wanakupa muda wa miaka 20, mkopo wa masharti nafuu unakudhuru nini, lakini maendeleo yanakuja haraka," amesema Rais Samia.

Rais Samia Suluhu Hassan, leo

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages