LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 13, 2021

DC SHEKIMWERI, VIONGOZI WA DINI WAIPONGEZA TGGA KUFANIKISHA MRADI WA KUELIMISHA MADHARA YA JI POMBE ULIOKITHIRI+video


Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri akipokea zawadi kutoka kwa Mratibu wa Miradi wa Chama cha Skauti wa Kike Tanzania (Tanzania Girl Guides Association, TGGA) Valentina Gonza baada ya kufunga rasmi mradi wa kutoa elimu kuhusu madhara yatokanayo na unywaji pombe uliokithiri ulioendeshwa na TGGA katika baadhi ya Kata wilayani humo.


 DC Shekimweri ambaye alikuwa mgeni rasmi aliipongeza TGGA kwa kufanikisha kwa mafanikio mradi huo kiasi cha baadhi ya wauza pombe kuacha kuuza na kuamua kufanya biashara zingine.


Pia TGGA ilipongezwa na wageni waalikwa wakiwemo viongozi wa dini ambao waliomba uongozi wa TGGA kufanya mipango ya kuendelea na mradi huo katika Kata zingine za jiji hilo la Dodoma.


Mratibu wa  Mradi huo, Valentina Gonza akielezea jinsi walivyoendesha mradi kuo katika Kata nne katika wilaya ya Dodoma.
Kiongozi wa dini Mwakilishi kutoka CCT, Ephraem Mbise akielezea madhara zaidi za unywaji pombe uliokithiri
Kisusu Mwagonga kiongozi wa dini kutoka Bakwata Mkoa wa Dodoma, akielezea jinsi kitabu kitukufu cha Quran kinavyokataza unywaji pombe.
Baadhi wa walimu na vijana wa kujitolea wa TGGA ambao walishiriki kutoa elimu wakati wa mradi huo. 
Baadhi ya wanafunzi walioshiriki kutoa elimu ya kuelezea madhara ya unywaji pombe uliokithiri.
Asha Juma mkazi wa Ndejengwa, Dodoma akielezea jinsi alivyochukua uamuzi wa kuacha kuuza pombe na  hatimaye kuanzisha biashara nyingine.
Diwani wa Kata ya Kikuzu Kusini Phillip Vumu akikabidhi zawadi kwa waliofanikisha mradi huo ikiwa ni sehemu ya TGGA kutambua mchango wao huo.





Philip Vumu naye akikabidhiwa zawadi na Valentina Gonza.
Mkufunzi wa TGGA Mkoa wa Dodoma, Mariam Mateleka akitoa shukrani kwa DC Shekimweri kwa kufunga rasmi mradi huo.
Phillip Vumu na Valentina Gonza wakiwa katika picha ya pamoja na watu mbalimbali ambao kwa namna moja ama nyingine walisaidia mradi huo kufanikiwa.




 PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA


Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Valentina Gonza akitoa taarifa ya mradi,DC Shekimweri na viongozi wa dini wakiipongeza TGGA....

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA 
MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM 
0754264203

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages