LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 16, 2021

BARAZA LA UWT MKOA WA DAR ES SALAAM, LAFANYIKA JANA, LAJADILI MAENDELEO YA UJENZI WA NYUMBA ZA WATUMISHI, HALI YA MIKOPO KWA WANAWAKE

 Katibu wa Jumuiya ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam Grace Haule akiwasilisha kwa Wajumbe Taarifa ya Jumla ya masuala mbali mbali wakati wa Kikao cha Baraza la UWT mkoa huo, lililofanyika katika Ukumbi wa Arnatouglou, jana jioni. Mambo aliyowasilisha ni pamoja ni pamoja na Hali ya Uhai wa Jumuiya hiyo, Maendeleo ya Ujenzi wa nyumba za watumishi wa Jumuiya hiyo na Hali ya Mikopo inayotolewa na Halmashauri kwa Wanawake. Kushoto ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Angel Akilimali na kutoka Kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa huo Mama Kate Kamba na Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Florence Masunga.
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Angel Akilimali (kushoto) na Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Florence Masunga, wakifuatilia kwa makini wakati Katibu wa UWT mkoa huo Grace Haule akisoma taarifa hiyo.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Mama Kate Kamba akifuatilia kupitia kabrasha, wakati Katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Grace Haule akisoma taarifa. Kushoto ni Mwenyekiti wa UWT mkoa huo Mama Florence Masunga.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni Anna Hangaya (Mama Makete) akifuatilia kwa makini wakati taarifa hiyo ikisomwa.
Mjumbe wa Baraza hilo, Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Dar es Salaam Janeth Mahawanga akifuatilia kwa makini wakati taarifa ikisomwa. Katika Taaifa hiyo Katibu wa UWT mkoa Grace Haule alisema Mbunge huyo ametoa mchango wa mifuko 100 kila Wilaya Dar es Salaam kusaidia ujenzi wa nyumba za Watumishi wa UWT.
Baadhi ya Wajumbe wakiwa na nakala za taarifa iliyokuwa ikiwasilishwa.
baadhi ya wajumbe wakiwa kwenye Baraza hilo.
Mbunge Stella Ikupa (kushoto) akifuatilia taarifa kwenye Kikao hicho. Katika Taarifa hiyo ilielezwa kuwa naye pia alitoa mchango wa sh. milioni moja kusaidia ujenzi wa nyumba za Watumishi wa UWT mkoa wa Dar es Salaam.
Wajumbe wakiwa kwenye Baraza hilo.

"Bila shaka wajumbe mmeisikia taarifa kama ilivyosomwa na Katibu wetu, haya kuna mwenye kuchangia jambo la kuchangia kwenye taarifa hiyo?" Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Florence Masunga akiwauliza wajumbe baada ya Grace haule (katikati) kusoma taarifa.
Wajumbe wakimsikiliza Mwenyekiti Mama Masunga.
Katibu wa UWT Temeke akitoa taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa nyumba ya Mtumishi wa UWT wilayani kwake.
Wajumbe wakishauriana jambo ukumbini.
Mwenyekiti wa UWT Kinondoni Anna Hangaya (kushoto), akielezea maendeleo ya Ujenzi wa nyumba ya Mtumishi wa UWT wilayani kwake.
Mbunge wa kuteuliwa (CCM) Janeth Masaburi akieleza changamoto ya urejeshaji wa mikopo ya Halmashauri kwa wanawake waliokopa, akashauri Jumuiya ikawatafutie mashamba katika mkoa wa Pwani Kinamama waliokopa ili wafanye kilimo cha pilipili kicha, akisema ila lipa sana kwa kuwa kilo moja ya zao hilo ni sh. 5000 ambayo haifikiwi na mazao mengine kama mahindi na korosho. Kulia ni Mbunge Janneth Mahawanga.
" Changamoto kwenye hii mikopo, unakuta watu hasa vijana wanaunda kikundi, wakishapewa pesa badala ya kukukuza mitaji yao, wanagawana pesa kila mmoja anaenda kununu smartphone!", sasa hapo inakuwa urejeshaji ni mgumu sana, Nashauri wakopaji wawe wanapewa kwanza elimu ya namna ya kuzitumia fedha za mikopo, mtu anakopa kwa ajili ya kuanzisha biashara, hivyo sivyo pesa ya mkopo ni ya kukuza mtaji, siyo ya kuanzisha biashara...", akasema mjumbe huyu kutoka Kigamboni.
"Sasa mimi nashauri, badala ya kuwapeleka jela hawa kina mama wanaoshindwa kurejesha mikopo, tutafute shughuli endelevu wanazoweza kufanya ili wapate pesa, kama kulima mashamba au kuwaanzishia viwanda, vianzishwe viwanda kama vya nguo au hata vya hizi rasta..", akasema Mama Kate Kamba baada ya mjumbe mmoja kutoa hoja kwamba wanaoshindwa kulipa wapelekwe wote jela.
Mwenyekiti Mama Masunga akihitimisha mjadala mwishoni mwa kikao kicho. Kushoto ni Mjumbe wa NEC Angel Akilimali na katikati ni Katibu wa UWT mkoa, Grace Haule.(Maelezo/Picha na Bashir Nkoromo, Blog ya Taifa ya CCM).

1 comment:

  1. Asante kwa kujali na kuweka kumbukumbu zetu. Kazi IENDELEE đź‘Ť

    ReplyDelete

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages