LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 24, 2021

WIZARA YA ELIMU NA CRJE WASAINI MKATABA KUANZA UJENZI WA JENGO LA KISASA OFISI ZA WIZARA MTUMBA+video


 Jengo la Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia likavyoonekana baada ya ujenzi wake kukamilika baada ya miaka miwili katika Mji wa Kiserikali wa Magufuli, eneo la Mtumba jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sazansi na Teknolojia, Dkt Leonard Akwilapo akitiliana saini mkataba na Mkurugenzi wa Mikataba wa Kampuni ya Ujenzi ya CRJE ya China, David Zhou kwa makubaliano ya kampuni hiyo kuanza ujenzi wa jengo la ofisi za wizara awamu ya pili katika Mji wa Kiserikali wa Magufuli eneo la Mtumba, jijini Dodoma. Mkataba huo umesainiwa leo Novemba 24, 2021 jijini Dodoma ambapo ujenzi wa jengo hilo utakamilika kwa miaka miwili na gharama ya ujenzi ni Sh. Bilioni 15.9. Wameteuliwa wasimamizi wa ujenzi huo ambao ni; Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) watakaopatiwa sh. mil. 687.2 na ABEC sh. mir.581.2.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt Leonarad Akwilapo akibadilishana hati hizo na Mkurugenzi wa Mikataba wa Kampuni ya Ujenzi ya CRJE ya China, David Zhou.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt Leonard Akwilapo akimkabidhi kitabu cha mwongozo wa ujenzi huo, Mkurugenzi wa Mikataba wa Kampuni ya Ujenzi ya CRJE ya China, David Zhou. Anayeshuhudia kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa wizara hiyo, Moshi Kabengwe.


Baadhi ya maofisa wa Kampuni ya Ujenzi ya CRJE.
Katibu Mkuu, Akwilapo akizungumza kabla ya kusaini mkataba huo.
Baadhi ya watumishi wa wizara hiyo.



 Katibu Mkuu, Akwilapo (katikati) akiwa na baadhi ya maafisa wa Kampuni ya Ujenzi wa CRJE pamoja na  Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa wizara hiyo, Moshi Kabengwe (kushoto),Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Carolyne Nombo  na Naibu Katibu Mkuu mwingine wa wizara hiyo, Profesa James Mdoe.


PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA


Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza/kuona kupitia clip hii ujue yaliyojiri wakati wa kutiliana saini mkataba huo...

Imeandaliwa na Richard Mwaikenda 
Mhariri Blog ya Taifa ya CCM 
0754264203


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages