Wakazi wa kata ya Tingiti wilayani Mpwapwa wakishangilia ujio wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bw.Antony Mtaka wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua miundombinu.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bw.Antony Mtaka,akikagua ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Tingiti wilayani Mpwapwa mara baada ya kufanya yake ya kikazi ya kukagua miundombinu.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka,akizungumza mara baada ya kumaliza mgogoro wa muda mrefu wa ujenzi wa shule ya Sekondari katika Vijiji vya Lugole na Tingita Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka,akisisitiza jambo kwa wananchi mara baada ya kumaliza mgogoro wa muda mrefu wa ujenzi wa shule ya Sekondari katika Vijiji vya Lugole na Tingita Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma.
Wananchi wakimsikiliza MKUU wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka,wakati akizungumza mara baada ya kumaliza mgogoro wa muda mrefu wa ujenzi wa shule ya Sekondari katika Vijiji vya Lugole na Tingita Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma,Dkt.Fatma Mganga,akizungumza na wananchi
Mkazi wa kijiji cha Tingiti,Peter Masuru,akimpongoza Mkuu wa Mkoa kwa kuitikia wito wao na kuweza kwenda kutatua tatizo hilo la muda mrefu.
……………………………………………………
Na.Erick Mungele,Mpwapwa
MKUU wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka amemaliza mgogoro wa muda mrefu wa ujenzi wa shule ya Sekondari ijengwe katika eneo lipi Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma.
Hatua hiyo imekuja kufuatia wakazi wa vijiji vya Lugole na Tingiti Wilayani Mpwapwa kila mmoja kutaka shule ya sekondari ijengwe katika eneo lake.
Mtaka ameutatua mgogoro huo kwa kuagiza shule hiyo kila Kata ijengwe katika kijiji chake cha Lugole na Tingiti huku akiahidi kutoa mifuko 200 ya Saruji pamoja na mabati 184.
Akizungumza na wakazi hao,wakati wa ziara yake Wilayani Mpwapwa,Mtaka amesema aina ya mgogoro ulipo ni wa maendeleo na jambo hilo limemfurahisha kwani wengi huwa na mabishano ya timu za Simba na Yanga tofauti na wao ambao wanagombania maendeleo.
“Hata wazazi wetu wanapozaa si huwa wanapata uchungu? uchungu unaenda wakishatuzaa uchungu unaendelea? Sasa viongozi tumeishakuja Mwenyekiti wa kijiji na wewe shusha mori.Sisi tumepita hapa nikaona watu wapo barabarani hata kama msingekuwa mmekaa hivi kwenye kurudi lazima ningesimama hapa.
“Mimi hapa ninapokutanishwa na jambo zuri ni tofauti namna ya kulielewa mkienda katika kuliewa hamtagombana hili ni jambo zuri la maendeleo cha kwanza ni nyinyi kutafsiri aina ya mgogoro ambao mnao ni wa maendeleo,
Aidha RC Mataka amesema kwanini wakazi hao wagombane wakati eneo la Lugole lina watoto wengi kuliko Tingiti hivyo ameagiza shule hiyo ijengwe katika eneo la Lugole.
“Kuanzia leo ugomvi umefanyaje? ( umeishaaaaaaaaa) kwahiyo Sekondari itajengwa hapa Lugole na kule Tingita watajenge shule yao kwahiyo kwa ridhaa yenu mshamaliza kila kitu panakuja panapimwa ili tuanze ujenzi ni lazima tuwe na hati wataalamu hii migongano haiwahusu sisi tunawahudumia wananchi.
“Mimi kwetu Musoma kijiji changu kinaitwa Suguti nawaambia habari za kwangu kwa sababu mambo ya Biblia siyajui, mwamko wa elimu hapa kwenu haujawa mkubwa sana ndio maana mnagombana lakini mimi ningekuwa ni mimi ningejenga shule yetu hapa ya sekondari.
“Kwanini tugombane nyinyi mna idadi mara mbili ya watoto wa Tingiti mnataka watoto 88 waliofaulu watembee mpaka kule, kijijini kwangu kila kitongoji kina shule,uchagani kule Moshi hakuna shule ya Kata,”amesema.
Aidha,Mtaka ameagiza eneo litakalojengwa shule hiyo waweke madarasa 16 pamoja na bwalo la chakula,mabweni viwanja vya michezo pamoja na eneo la bustani na ofisi za walimu.
“Mambo ya msingi watu ambao wanahangaikia maendeleo yao wapo wachache tujipongeze watu wengi wanashindana mambo ya Simba na Yanga nyinyi mnashindania kujenga shule ni watu wachache? Hii hasira tuihamishie kwenye maendeleo mimi nitawaunga mkono,”amesema.
Naye,Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma,Dkt.Fatma Mganga, amewataka wakazi wa Wilaya hiyo, kuwekeza katika kilimo cha Alizeti kwani Serikali imetoa mbegu bora huku akidai Serikali ya Mkoa itaendelea kutoa ushirikiano kwa wakulima wa zao hilo.
“Kutokana na mazingira yetu yanaruhusu kulima na ni sehemu nzuri serikali imetoa mbengu bora za alizeti kwahiyo nivyema mkawekeza katika kilimo hicho pia kutoka na serikali inahitajii sisi Dodoma tutoe eneo kubwa la zao hili,” amesema
Kwa upande wake,mkazi wa kijiji cha Tingiti,Peter Masuru amempongoza Mkuu wa Mkoa kwa kuitikia wito wao na kuweza kwenda kutatua tatizo hilo la muda mrefu.
Amesema kumalizika kwa jengo la shule litasaidia wanafunzi kusoma kwa karibu na kuwaondolea adha ya kutembea kwa muda mrefu.
“Tunampongeza mkuu wa mkoa kuweza kusikiliza wito wetu na kuja kutuondolea tatizo hili la muda mrefu maana ametusaidia wengi,”amesema.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇