LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 10, 2021

RAIS SAMIA KUONDMKA NCHINI LEO KWENDA MISRI KUFANYA ZIARA YA SIKU TATU NCHINI HUMO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Novemba 10, 2021 anatarajiwa kuondoka nchini kwenda Cairo nchini Misri kwa ajili ya ziara ya Kiserikali ya siku tatu.
 
Taarifa iliyotolewa jana jioni na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Jaffar Haniu imesema ziara hiyo ya inafuatia mwaliko wa Rais wa nchi hiyo, Abdel Fattah Al Sisi.

"Katika ziara hiyo, Rais Samia pamoja na mambo mengine anatarajiwa kufanya mazungumzo na mwenyeji wake katika maeneo kadhaa ya ushirikiano kati ya Tanzania na Misri ikiwemo nyanja za diplomasia, uchumi, siasa, elimu, utalii na huduma za kijamii.

Rais Samia na mwenyeji wake pia wanatarajiwa kushuhudia utiaji saini mkataba mmoja na hati saba  za makubaliano kati ya Tanzania na Misri", imesema taarifa hiyo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages