LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 22, 2021

PROF. MUSERU AONGOZA WAOMBOLEZAJI KIFO CHA MFANYAZI HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

      Enzi za Uhai wake Ally Lidengi 

 Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru awaongoza wafanyazi Hospitali ya Taifa Muhimbili, ndugu na jamaa na marafiki kuuaga mwili wa aliyekuwa Mfanyakazi wa Hospitali hiyo leo Novemba 22, 2021. 

Nasimama hapa kwa niaba ya Bodi ya Wadhamini, Wafanyakazi na Jumuiya ya Muhimbili na mimi naomba niseme machache, Ingawa tukio hili ambalo tupo hapa hutokea katika maisha ya mwanadamu kama alivyotukumbusha mtumishi wa Mungu ni tukio lisilo zoweleka inabidi tuishinalo linapo tokea hivyo tumshukuru Mungu  alisema Museru;.

Napendakutoa pole kwa kwa familia ya marehemu najuwa hapa tunaaga Mume, Baba, tunaaga Babu, Mjomba Rafiki na ninajuwa kutakuwa na uchungu na kujiuliza maswali mengi kwa kuondokewa na mpendwa wetu hivyo basi tunaomba tumuachie Mungu na tujuwe kwamba maazimio yake yametimizwa kwa mwenzetu aliyetutoka hivi karibuni Mkoani Morogoro mnamo Novemba 20, 2021 wakati akishiriki Mchezo wa kuvuta kamba (SHIMMUTA 2021).

Kwa wafanyakazi Hospitali ya Taifa Muhimbili Marehemu kama tulivyosema tumekaanae takribani miaka thelathini na tumetoa ushuhuda marehemu alikuwa mchapakazi alikuwa na tabia ambayo mtu anaitaka kwakila mfanyakazi awenayo hivyo tumempoteza mfanyakazi mwenzetu hodari, tumepoteza rafiki,lakini yote hayo ni ya mungu  aliendelea kwa kusema

Ninaamini kwa Mwenyezi Mungu aliyeamua na ninawaomba kwa wafanyakazi tumuenzi mwenzetu kwakutenda yale mazuri aliyokuwa akiyatenda ilikusudi tuendelee kutoa huduma ile tunayotakiwa kuitoa na sisi kama Hospitali ya Taifa Muhimbili msiba huu umetugusa napia tupo pamoja na familia naomba kutoa shukrani zetu kwa SHIMMUTA kwani wamekuwa karibu nasi toka tukio hili lilipotokea na wamemtuma mwenzao na  kusimamisha michezo kwa siku kadhaa kwa ajili ya kumuenzi mwenzetu.

Hivyo tuzidi kumuombea mwenzetu na mwisho Bodi ya Wadhamini inawatakia safari njema na maziko mema na kuzidi kumuomba na Mungu aweze kuwarudi salama  kwa wale watakaoweza kubahatika kuondoka na mwili amina. 

HAKIKA SISI SOTE NI WA MWENYEZI MUNGU NA KWAKE TUTAREJEA.

 

Mwenyekiti TUGHE Tawi la Muhimbili Mziwanda Chimwege (wa tatu kulia) akijumuika na baadhi ya Wafanyakazi wenzake wakati wa kumuombea Dua mfanyakazi mwenzake Ally Lidengi  



Baadhi ya Wafanyakazi Hospitali ya Taifa Muhimbili na ndugu na marafiki wakiwa wamebeba jeneza lenye mwilki wa aliyekuwa mfanyakazi Hospitali ya Taifa Muhi,mbili, Ally Lidengi
Baadhi ya Wafanyakazi Hospitali ya Taifa Muhimbili na ndugu na marafiki wakiwa wamebeba jeneza lenye mwilki wa aliyekuwa mfanyakazi Hospitali ya Taifa Muhi,mbili, Ally Lidengi

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages