LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 29, 2021

MAHAFALI YA 4 YA VYUO VYA KIMATAIFA VYA CORNERSTONE NA HHWBC YAFANA UDOM+video

 


Mahafali ya 4 ya vyuo vikuu vya Kimataifa vya Cornerstone na HHWBC vya Marekani yamefana ambapo Watanzania wanaosoma kwa njia ya mtandao katika vyuo hivyo wametunukiwa Diploma, Digrii ya Awali, Digrii ya Umahiri, Digrii ya Udaktari wa Falsafa na Digrii ya Udaktari wa Heshima. Aliyekuwa anawatunuku ni Mkuu wa Mafunzo wa vyuo hivyo, Profesa Rejoyce Ndalima katika hafla iliyofanyika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Novemba 27, 2021..

Pichani Profesa Ndalima akimkabidhi cheti Gabriel Nderumaki baada ya kumtunuku Udaktari wa Falsafa, kwa kutambua mchango wake katika Maendeleo ya Jamii, ambapo kupitia katika mashindano aliyo yaasisi ya mbio za Rock City sehemu ya mapato huwasaidia watu wenye ulemavu wa ngozi mkoani Mwanza.
Wahitimu wakiongozwa na Bendi ya Jeshi la Kujenga Taifa wakiingia ukumbini kutunukiwa.
Mwanamuziki mkongwe, Cosmas Chidumule akikabidhiwa tuzo kwa kutambua mchango wake wa kueneza injili kwa njia  nyimbo.
Askofu, Dkt Evance Chande akijadiliana jambo na mmoja wa viongozi wa vyuo hivyo wakati wa mahafali hayo.
 
Profesa Ndalima akimkabidhi cheti Paul Siyame baada ya kumtunuku Udaktari wa Falsafa
Mkurugenzi wa zamani wa Chama cha Waandishi Wanawake Tanzania (TAMWA), Ananilea Nkya akimpongeza Hellen Usiri ambaye ametunukiwa Udaktari wa Falsafa wa Heshima kwa kutambua mchango wake kwa jamii.
Hellen Usiri akikabidhiwa cheti na Profesa Ndalima baada ya kumtunuku Udaktari wa Falsafa wa Heshima kwa kutambua mchango wake kwa jamii.


Profesa Ndalima akimkabidhi cheti Askofu Edwin Yona baada ya kumtunuku digrii ya umahiri katika mahafali hayo.



PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA


Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza/kuona kupitia clip hii ya video  yaliyojiri katika mahafali hayo...









IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA 
MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
 0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages